Download Mp3 from African

EXCLUSIVES | Jay Moe aeleza jinsi alivyopata aibu baada ya kumdharau Billnass

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nisaidie Kushare’ amesema licha ya kutamani kufanyakazi na rapa wa wimbo ‘Sitaki Mazoea’, Billnass lakini hatasahau alivyomdharau kabla ya kusikiliza na kuona video zake.
Rapa huyo amedai kabla ya kumwona, kusikiliza na kutazama video zake hakuwa akijua uwezo mkubwa alionao rapa huyo hivyo hata alipotumiwa wimbo wa rapa huyo na meneja wake alidharau hakuusikiliza hadi walipokutana nchini Afrika Kusini.
“Unajua kuna siku meneja wake, Bill Nas ‘Mchafu’, alinitumia wimbo akiniomba niwatumie na wengine lakini mimi sikufanya hivyo, nilipowakuta Afrika Kusini na kuwahoji wakaniambia wapo kwa ajili ya kufanya video ya wimbo alionitumia, nilijisikia vibaya sana na niliona aibu maana niliona video yake ni kali tofauti na nilivyokuwa nikimdhania,” Jay Moe alimwambia Kuluti Mc mwandishi wa mtandao huu wa africanmishe.com (Mishe Mishe Media)
“Hapo nikajifunza kitu kuwa hutakiwi kumdharau mtu, maana dogo ana uwezo mkubwa wa kurap na anajua nini anafanya hadi nimemwahidi kufanya naye kazi,” alisema Jay Moe.
Rapa huyo amedai kwamba licha ya kutamani kufanya naye kazi pia anatamani kumtungia mashairi Billnass kama atakuwa tayari.
Back To Top