Download Mp3 from African

Alichokisema Kocha wa Vital'o baada ya kuitambia Inter Star (1-3)

Kocha mkuu wa timu ya Vital'o, Haringingo Christian Francis Mbaya baada ya kuitambia timu ya Inter Star Jumamossi wiki hii kwa kuifunga mabao 3-1 katika mechi ya kwanza ya marudio ya Ligi kuu Primus League, amesema kuwa atahakikisha wanapata pointi tatu kwa kila  mechi kupunguza tofauti ya pointi kati yao na timu mbili Atletico Olympic na LLB.

Mbaya baada ya kuanza vibaya mwanzoni mwa Ligi Kuu kwasasa alijaribu kurejesha kiwangu cha timu tofauti na awali, wakati klabu mbili zikiwa mbioni kwa kutwa ubingwa msimu huu, kocha Mbaya wa Vital'o alisema kamwe wasidanganyike kuhusu kutwa ubingwa wa Ligii Kuu msimu huu wakati bado  mechi za marudio ndio zinaanza na kila timu ingali na bahati ya kuwa bingwa.

Aidha siri ya mabadiliko ya timu hiyo, kocha Mbaya alisema kuwa mambo mengi yalitokea tukapoteza mechi kadhaa mwanzoni mwa ligi ila ninaamini tutafanya vizuri  baada ya maandalizi ya uhakika. tumebadilika kidogo hasa katika mbinu ili tuweze kupata pointi tatu zitakazo tuwezesha kumaliza wa kwanza kwenye Ligi kuu na pia kufanya vizuri katika michuano za kimataifa ambayo mnafaham kama mechi ya awali tutakuwa ugenini.
Back To Top