Download Mp3 from African

Msanii Nay wa Mitego Amlilia Mwanamke Aliyedhalilishwa kwa kuchapwa Viboko

Rapa
Nay wa Mitego ameonesha kusikitishwa na moja ya video ambayo
inamuonesha mwanamke akiwa amezungukwa na wazee na vijana wengi
wakimchapa viboko kama adhabu kutokana na makosa ambayo mwanamke huyo
ameyafanya.


Rapa
Nay wa Mitego baada ya kuitazama video hiyo amefunguka na kusema licha
ya ubabe wake na ukorofi wake lakini katika maisha yake hajawahi kumpiga
mwanamke na kusema anawachukia sana wanaume ambao wamekuwa wakiwapiga
wanawake.

"Na
ubabe wangu wote, sijawahi kumpiga mwanamke, namchukia mwanaume yoyote
kwenye hii dunia anaye mpiga mwanamke. Ningekua ni kiongozi kwenye hii
nchi hawa mbw*** wote wangeenda jela bila mjadala, acha jela ikajae
lakini cha moto wakione. Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu. Sijui kabila
gani hawa mashetani..!! eeh Mungu walaani hawa binadamu
wanaomdhalilisha huyu mama, wageuze ata funza tu. Wahusikaaaaa delight
chukue hatua kali juu hili". Alisisitiza Nay wa Mitego

Tazama hapa video ya mwanamke huyo, akiadhibiwa na kundi la wanaume...
Tag : lainnya
Back To Top