Msanii wa kike wa muziki kutoka Burundi, Natacha maarufu kama la Namba ao La Bamba, ambaye alirejea vizuri nchini Februari 12, akitokea Geneve kwa kufanya show, alifunguka mbele ya watangazaji na kusema kuwa Uzalendo ni jambo la muhimu sana pindi unapokua nje ya nchi ukitangaza bendera ya nchi yako kupitia kazi zako.
Nilipo kuwa Geneve kwa kweli nimefurahi kwa mapokezi na hawakupenda niondoke, kuna kitu muhimu kinachotuma ujulikane bila kuulizwa swali ukiwa ugenini. Najua kila mtu kufanya mambo yake apendavyo ili mradi tu havunji sheria za nchi, kwa kuzingatia hilo nimeweza kutangaza na wakaelewa nimetokea nchi gani bila kuulizwa swali pindi walipo niona navaa nguo ikiwa na jina la Bujumbura. imekuwa ni nafasi kubwa sana yenye heshima ya mimi kutoka Republic of Burundi nikiwakilisha pia Afrika Mashariki. Nawaomba wasanii wenzangu kuwa wazalendo pindi wanapo pata bahati ya kuwakilisha nchi yawo nje ya nchi kwa kuonesha wanatokea wapi bila kusubiri wakuulize maswali.
Mwana mama Natacha anazidi kufanya vizuri kwenye ulimwengu wa muziki wa Burundifleva ndio sababu anazidi kupiga hatua za kufanya demonstrate nje ya nchi.
''Ndiyo ninaimani wameona au wameuliza nani anayefanya vizuri nchini wakaona ni La Namba ndio sababu wamenialika kwenda kufanya demonstrate na pia sio mwisho nitazidi kufanya zingine nje ya nchi. Kwa kumalizia naomba ni chukue nafasi hii kuwashukuru warundi wote kwa kunisapoti katika kazi zangu, na kwa wote mlionipokea, nawashukuru mno sina cha kuwalipa zaidi ya kusema Ahsante sana huu ni mwanzo mpya'', Alisema natacha La Namba.