Msanii King Moses Vyizigiro wa Burundifleva kutoka Republic of Burundi mwenye makazi yake nchini Marekani, sasa limekua jina maarufu katika masikio ya warundi, Afrika Mashariki na kwingineko hasa baada ya kuachia wimbo wake Chou Chou akishirikiana na Akes Don.
Kwasasa kwenye mitandao ya kijamii kama Tweeter, facebook, Instagram na hata Whatsapp lazima utakutana na jina la King Moses ikiunganishwa na Akes Don kwa kazi ''Chou chou'' na wengine wataunganisha na B-Face kwa kazi nzuri anazo zidi kufanya.
Anafahamika kama King Moses Vyizigiro, amezaliwa mwaka 1991 mkoani Gitega nchini Burundi, baada ya miaka tisa (9) alikumbwa na ugonjwa wa kushindwa kuongea na kusikia.
Mwaka umoja akipata matibabu mjini Bujumbura bila mafanikio, alifanikiwa kupelekwa nchini Nigeria kwa matibabu zaidi.
Baada ya kutibiwa nchini Nigeria bila mafanikio miaka kadhaa, akiwa na umri wa miaka 19, kama miujiza ya Mungu aliamka akaanza kusema na kusikia ndipo alipelekwa Marekani mwaka wa 2013 na kuteuliwa kama balozi wa ma Bubu Afrika Mashariki.
Historia yake kimuziki inaonesha King Moses alianza kuimba akiwa na umri mdogo (19) wakati akisoma shule ambapo alikua akitoa burudani katika matamasha ya muziki yaliyokuwa yakiandaliwa na wafanyakazi wa shule, wakati wa hafla za mwishoni wa mwaka na katika mashindano mengine ya jumuiya akiwakilisha shule yake.
Wakati amekulia mbali na nchi yake, hakuacha mapenzi yake kwenye muziki. Kwasasa ananyimbo kumi (10) za well na tatu (3) za video huku akizidi kutamba na kibao chake aliyoipa jina la Chou Chou akimshirikisha Akes Don.
Baada ya kufanya vizuri kwenye muziki mwishoni na mwanzoni mwa mwaka 2017, King Moses anachukulia muziki kama kazi na kuipa nafasi kubwa kwenye arakati zake zote na kwasasa anazidi kutoa nyimbo za kuvutia tofauti na awali.
King Moses ana ndoto ya kufungua miradi mingi ya kusaidia watu wasiojiweza na kuzidi kujijenga kimuziki ili siku za mbele mashabiki wa Burundifleva waweze kujivunia jina lake.
Habari zake kuandikwa katika mitandao ya kijamii pamoja na shughuli zake za uhisani zimesababisha wengi kudai kuwa anataka tu umaarufu, kujulikana na kuzungumziwa kila wakati. Hata hivyo akijibu madai hayo, King Moses alisema umaarufu unamtafuta yeye na sio kwamba yeye anautafuta na kuongeza kuwa hakutegemea sana muziki, kwasasa amegundua kuwa anakipaji cha muziki na muziki ni kazi kwake.
Tuwakumbushe kuwa moja ya arakati zake kwenye muziki hivi karibuni, Moses anatarajia kuachia video ya wimbo wake mpya, hata hivyo hakupendelea kutaja jina la wimbo huku akiwataka mashabiki zake wakae mkao wakula kwa kusubiria ujio wa kazi yake mpya.