Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Serikali imeombwa iwafikirie wauzaji wadogowadogo wa madini ya Tanzanite mkoani Manyara na Arusha , kwenye ulipaji wa tozo ya kodi kwa asilimia eighteen kwani kodi hiyo inalengo la kuwamaliza wafanyabiashara wadogowadogo wa madini hayo.
Akizungumza kwenye mnada wa vito wa madini ya Tanzanite, Mwenyekiti wa mabroka mkoa wa Arusha,Jeremia Simioni alidai licha ya kodi kuwa kihalali kisheria lakini ni wazawa pekee ndio wanaotakiwa kulipa kodi hiyo
Alisema ipo sababu ya serikali kukangalia namna ya ulipaji wa kodi hiyo,aidha kuiondoa kabisa ama na wafanyabiashara wageni nao wakapangiwa namna ya kulipa kodi hiyo
"Utamkuta mfanyabiashara ananunua mawe fifty milioni na anaekewa VAT kwa asilimia eighteen au zaidi chakushangaza mgeni atanunua mawe kwa kiasi hicho au zaidi lakini hatozwi VAT hiyo,"alisema Jeremia
"Sasa jamani inakuaje mzawa alipe kodi lakini mgeni asilipe kodi yeye anafanya biashara kama ni bure kwakweli serikali ilitizame hili sasa, "alisema Jeremia
Hata hivyo alisema pamoja na serikali kudai kuwarudushia baadhi ya malipo hasa kwa wafanyabiara wanaosafirisha madini hayo bado utekelezaji huo haujaanza
"Hajawahi kulipwa mtu,sisi tunataka aidha tozo iondolewe ama tulipe wote ,"alisema Jeremia
Sambamba na hayo ameiomba serikali iwaandalie mnada wafanyabishara wa madini wadogowadogo ili nao waweze kukua kwenye biashara hiyo
"Mnada mzuri lakini huwezi kuchanganya wafanyabiashara wakubwa na wadogo,sisi tunaiomba serikali iandae mnada kwaajili ya wafanyabaishara wa madini wadogowadogo,"alisema Jeremia
Mbunge wa Simanjiro,James Olemilia ameitaka serikali kuhakikisha mjinj wa Manyara unapotokea madini ya tanzanite unakua
"Simanjiro pamoja na kuwa linatoa madini ya tanzanite ambayo yanategemewa na mataifa mbalimbali lakini bado maisha magumu,hakuna Zahanati,shule ,tunataka madini hayo yainufaishe kwanza simanjiro,"Alisema James
Mkuu wa mkoa wa Manyara Joel Bendera alidai ipo sababu ya serikali kuangalia namna ya kuhakikisha wachimbaji wadogowadogo wa madini wananufaika
Amesema kuwa Mkoa wa Manyara haswa Simanjiro ni mkoa ambao unaongoza kwa maambukizi virusi vya ukimwi pamoja na TB
"Afya wa wachimbaji lazima izingatiwe ni asilimia nineteen ya wakazi wa manyara wanavirusi vya ukimwi,tb iko juu sana ,"alisema Bendera
Hata hivyo kutokana na mnada huo,Mkurugenzi wa TANSORT Arichad Kalugendo, alisema faida ya marabaha yaliyouzwa ni ix bilioni,huku serikali ikopokea tuzo kwa zaidi ya 400 milioni huku wilaya ya simanjiro ikinufaika kwa kiasi cha shilingi 26 milioni
Tag :
lainnya