Download Mp3 from African

Watanzania 132 Wakamatwa na Kufukuzwa Msumbiji, Kinamama Wabakwa

Maputo, Msumbiji. Takriban raia 132 wa Tanzania wanaoishi nchini Msumbiji wametimuliwa  nchini humo huku wengine wasiojulikana wakidaiwa kukamatwa kufuatia operesheni ilioanzishwa na serikali ya taifa hilo.
Kulingana na serikali ya Msumbiji operesheni hiyo inalenga kuwatimua raia wa kigeni wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
 Watanzania wamelalamika kufanyiwa vitendo vya unyanyasaji huku wanawake wakibakwa, kunyang’anywa pasipoti na kuchanwa. Pia, Watanzania wamelalamika askari wa Msumbiji wamekuwa wakipora mali zao na kuziharibu.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, imesema kuwa raia waliofukuzwa ama hata kukamatwa ni wale wanaoishi mji wa Monte Puez kwa kuwa una raia wengi wa kigeni ikilinganishwa na miji mingine.
Kulingana na taarifa hiyo tayari ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji unaendelea kufanya mawasiliano ya kidiplomasia na serikali ya Msumbiji ili kuwahakikishia usalama raia wa Tanzania na mali yao nchini humo.
Inakadiriwa kuwa, Watanzania wapatao elfu tatu (3,000) wanaishi na kufanya shughuli za kiuchumi na kijamii katika mji huo wa Monte Puez.
Hatua hiyo inajiri licha ya mataifa ya Msumbiji na Tanzania kufanya mkutano wa kuainisha maeneo ya ushirikiano yakiwemo maswala ya kibiashara na uhamiaji.

Wakati operesheni hiyo ikiendelea serikali ya Tanzania imekuwakumbusha Watanzania wote waishio ughaibuni, kufuata Sheria na taratibu za nchi hizo wanazoishi.
Tag : lainnya
Back To Top