Baadhi ya wafuasi wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)wakiwa wamevaa tisheti wakiwa na mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema baada ya kupewa dhamana.Picha na Vero Ignatus blog. |
Na Vero Ignatus,Arusha
Hatimae Mahakama kuu kanda ya Arusha imemuachia kwa dhamana Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbles Lema baada ya kusota rumande kwa miezi minne
Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana ya sh milioni moja pamoja na wadhamini wawili wenye vitambulisho vinavyotambulika na serikali
Akisoma hukumu ya Mbunge Lema katika Mahakama Kuu Arusha Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Salma Magimbi amesema kuwa Mbunge Lema hakupaswa kukaa mahabusu kwa muda mrefu kwani ilipaswa kupewa dhamana.
Jaji magimbi amesema kuwa wanamwachia lema kwa dhamana hiyo ya milioni moja ambapo kiasi hicho kimetolewa kwa njia ya bondi huku wadhamini wawili nao wakiwa na vigezo vya dhamana.
Akizungumza nje ya Mahakama hiyo Mbunge Lema amesema kuwa Jamhuri ilikuwa na nia ya kumfunga lakini mungu amempigania mpaka kutoka huku akimshukuru mke wake kwa jinsi alivyomfariji kwa kipindi akiwa ndani.
Lema amesema kuwa Alisema kwa sasa ameandaa waraka wa kumwandikia raisi kuwa wapo watu wanaoteseka bila kuwa na hatia magereza na kwamba atautoa siku za hivi karibuni
Nae wakili mtetezi wa Lema, Peter Kibatala amesema kuwa Mahakama kuu imelekeza kuwa mahakama za chini zisimamie madaraka yake na mamlaka yake bila kuyaachia na hivyo kwa sasa wanatakiwa kujiandaa kwa ajili ya kupambana na kesi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe amesema kuwa wanamkaribisha tena Lema Bungeni na kwamba kamati ya chama imemaliza vikao vyake mjini hapa na kuwashukuru wabunge wa mikoa mbali mbali waliofika kutetea dhamana ya lema.
Aidha Mbowe amelaani vikali kitendo cha jeshi la polisi kutumia mamlaka yao vibaya kwa kuwapiga wananchi bila makosa kwa madai kuwa wanakuja kuleta vurugu huku lengo ni kuja kusikiliza mbunge wao.
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akishuka kutoka kwenye gari ya magereza tayari kwa kuyingia mahakamani.Picha na Vero Ignatus Blog
Waziri mkuu mstaafu mhe,Edward Ngoyai Lowasa akiwa nje ya mahakamabaada ya mahakama kutoa muda wa dk fifteen kwa upande wa serikali kuombakuomba kuwasilisha hati zao za msingi na upande wa utetezi kusema wataijibu baada ya saa moja ambapo upande wa jahmuri walisema watatoa uamuzi saa saba na nusu
Tag :
lainnya