Watu wawili maarufu nchini Burundi Niyonzima Omary na Abdul Misambano wamefikia kujiunga na kufanya kazi pamoja kwa kuunda kundi ikibeba jina la Umoja Band ambayo ni muungano wa wanamuziki wa Mwambao au Taarabu kutoka Burundi.
Kundi hilo imeanzishwa hivi karibuni na kudhaminiwa na Niyonzima Omary maarufu kama Papa Fololo ambaye ni meneja na akiwa msemaji wa kundi hilo, Abdul Misambano ndie mwenyekiti wa kundi.
Aidha, viongozi wengine wanaounda kamati ya kundi hilo ni pamoja na mpiga solo mkongwe hapa nchini Burundi, Issa Jesus ambae ni Naodha wa kundi, mshauri mkuu ni Athumani Miraji, mwenyekiti wa heshima ni Abas Abako pamoja pia na Bwana mipango ambae ni Amani Yaoo.
Tuwafahamishe kwamba mpaka sasa wamefanikisha kufanya wimbo wa amani ambao ni fikra kutoka kwa Mwenyekiti wa kundi Abdul Misambano huku wakiwa na mipango wa kurikodi nyimbo nne (4) za ushirikiano.
Kinyume na kazi ya muziki kwasasa wametengeneza T-Shirt na kofia zenye nembo za kundi hilo na kufadhiliwa na mzee Omary Niyonzima, kama unavyo shuhudia picha hapa chini.