Mchezaji wa kati wa klabu ya Inter Stars ya daraja ya kwanza Primus League nchini Burundi, Hussein Ntahoturi alifikishwa hospitalini Ijumaa wiki hii, huku akizidiwa sana na akishindwa kusimama vizuri wala kula pekee yake.
Hussein Ntahoturi aligundulika anasumbuliwa na kiuno na homa ya matumbo (typhoid), hivyo akawa anapata matibabu na kuendelea na shughuli yake ila Ijumaa alizidiwa na kupelekwa kulazwa hospitalini.
Kiungo fundi wa klabu ya Inter Stars, Hussein Ntahoturi hali yake sio mbaya sana kwasasa na amelazwa katika hospitali ya La Reference maarufu kwa Dokta Mwamedi Juma Kariburyo(Buyenzi 10/37).
Mchezaji huyo ambaye wakati fulani alikua akijitoa muhanga mpaka kucheza anaumwa ili kuisaidia klabu yake katika ligi kuu, ni kwamba hali hii mchezaji anahitaji msaada na uangalizi wa karibu sana wa watalaam wa afya na viongozi, ndugu na marafiki.
Mke wa mchezaji Hussein anayezidi kutamba na klabu ya Inter Stars, alisema mumewe anahitaji msaada zaidi ili kufanikisha matibabu yake.