Kikosi cha Mbeya City
Meneja wa Mbeya City Godfrey Katepa amesema hali za nyota wa timu yake iko vizuri kabisa tayari kwa mchezo jambo linaloashiria kuwa hakuna kitakachowazuia kuibuka na ushindi dhidi ya wageni wao Toto African.
“Hali ya kikosi chetu ni zuri kabisa, hakuna mchezaji yoyote aliye majeruhi, Haruna Shamte aliyekuwa na maumivu ya kifundo cha mguu amerejea kikosini baada ya matibabu ya siku kadhaa jopo la madaktari wetu wametuthibitishia kuwa yuko sawa tayari wa mchezo wa leo, ni wazi hakuna kinachotuzuia kushinda,” amesema kimbe.
Kuhusu suala la wachezaji wa kigeni, Katepa amesema tayari hatua zimeshachukuliwa hivyo mashabiki wao wasiwe na wasiwasi juu ya kuwepo kikosini kwa wachezaji wao wanaotoka nje ya nchi.
“Viongozi wameshalichukulia hatua, kila kitu kimeshakamilishwa hivyo niwatoe wasiwasi mashabiki juu ya kocha na wachezaji wao kutoka nje,taratibu ziko sawa na watashiriki mchezo wa leo, waje uwanjani kwa wingi kwa ajili ya kuisapoti timu yao na wategemee ushindi kwa sababu tunataka kushinda ili tutoke kwenye nafasi tulipo sasa katika msimamo wa ligi na kusogea juu zaidi,” amesema Katepa.
Akiendelea zaidi Katepa aligusia suala Mrisho Ngassa kuwa bado halijakamilika kwa maana ya kufika kwa ITC yake lakini uongozi unaendelea kufanya mawasiliano na klabu ya Fanja ya Sultanate of Oman kuhakikisha suala hilo linakamilika ili nyota huyo aweze kuitumikia Mbeya City kwenye michezo inayofuata.
“Ni wazi ataukosa mchezo huu, suala lake bado halijakamilika, jambo muhimu ni kuwa uongozi bado unaendelea kufanya mawasiliano na klabu ya Fanja kuhakikisha linakamilika ili aweze kuichezea timu yake mpya kwenye michezo ijayo, awali walitutumia TPO pekee, hivyo tunasubiri RELEASE LETTER kutoka kwao ili tuweze kupata ITC kwa mujibu wa taratibu, ilikuwa watutumie jana lakini mtu ambaye alipaswa kufanya hiyo kazi alikuwa nje ya Oman,” amesema Katepa.
Katepa amesema, hawana mgogoro wowote na Fanja kama inavyoripotiwa na mawasiliano kati yao ni mazuri kama ilivyo kwa Shirikisho la Soka nchini TFF na Chama cha Soka nchini Sultanate of Oman hivyo siku si nyingi suala hilo litafikia mwisho.
Tag :
lainnya