Download Mp3 from African

Sallam Sk Meneja wa:Diamond Platnumz amefunguka kwa kusema Ommy Dimpoz anamjua zaidi Diamond Platnumz kuliko mimi.


Meneja

Meneja wa Kimataifa wa Mwanamuziki Diamond Platnumz, Sallam Sk amefunguka kwa kusema kuwa Muimbaji Ommy Dimpoz anamjua zaidi Diamond Platnumz kuliko yeye. Akiongea kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times Fm jana usiku, Meneja huyo amedai kuwa hawawezi kuingilia tofauti walionayo Ommy Dimpoz na Diamond Platnumz kwa kuwa Wanajuana kitambo kabla yake. “Mimi huwa naweka sana utani mitandaoni, Ommy Dimpoz anamjua Diamond zaidi kuliko mimi, sio kumbembeleza eti Ommy amuombe msamaha Diamond kwa faida gani hasa ninayoipata au nitakayopata kutoka kwake? aende mwenyewe akaombe Msamaha” alisema Sallam.

Tag : lainnya
Back To Top