MSIMLIAJI: Kuluti MC
“Una ushahidi wowote kama alitaka kumuua?” Shangazi aliniuliza nilipomuelezea kila kitu kuhusu ndoa yangu na kilichotokea siku ile.
“Hapana shangazi ila nahisi tu, kwanini mtoto alie na akutulia, halafu kwanini afunge mlango. Kuna mambo mengi yanaendelea shangazi na yananipa wasiwasi sana. Lazima kutakuwa na kitu kibaya alitaka kumfanyia mwanangu”
“Mwanangu ndoa ni uvumilivu, huwezi kumshutumu mume wako mambo kama hayo..!” Shangazi aliongea kwa sauti ya juu kama vile ananifokea. Nilistuka kwani nilitegemea kwa niliyomueleza atakuwa upande wangu.
“Shangazi sio kama namshutumu. Mume wangu kanifanyia mengi mabaya navumilia. Hili siwezi kuvumilia, isitoshe anasema mtoto si wake na nahisi hiyo ndiyo sababu ya kutaka kumuua?”
“Tema mate chini mwanangu, hayo unayonena ni makubwa! Mumeo hawezi kufanya hivyo na kama anasema mtoto si wake labda kuna vitu umefanya unanificha, mtu hawezi kuibuka na kusema tu mtoto si wake… lazima kuna kitu umefanya hutaki kuniambia”
Maneno ya shangazi yalinikatisha tamaa kabisa, nilishajiandaa kuondoka na kuanza maisha yangu upya bila ndoa lakini nilihitaji shemu ya kuanzia. Nilimuomba shangazi kukaa pale kwa muda wakati nikijipanga lakini alikata akisema. Aling’aka na kuona kam anilikua nataka kufanya kitu cha ajabu sana.
“Wewe ni mke wa mtu, siwezi kukuruhusu kukaa kwangu tu! Unafikiri Baba yako atanielewaje akijua mimi ndiyo nimevunja ndoa yako? Tatizo kidogo unataka kuondoka, unajua sisi kuna mangapi makubwa tumepitia? Unafikiri kila mwanamke anayekorofishana na mume wake angeondoka kungekua na ndoa kweli?
Mume wako kama kakuchoka akurudishe kama alivyokuchukua, unafikiri ukikaa hapa wazazi wako watanielewaje? Kaka atanielewa kweli kama mimi ndiyo nakuendekeza! Hapana, rudi huko huko na kama mumeo akikuleta hapa nitakupokea lakini huwezi kuja tu mwenyewe nikakupokea bila mumeo eti ndoa imekushinda.
Tena na shutuma kama hizo! Hata wazee hawjaashirikishwa! Hapana siwezi! Wewe ulikabidhiwa kwa mume hukujiondokea tu nyumbani kama kichaa! Maisha hayaendi hivyo mwanangu! Jifunze kuvumilia, ndoa zote zipo hivyo!”
Aliongea maneno mengi kiasi cha kushindwa kuendelea kumsikiliza tena, kusema kweli nilichanganyikiwa, nilibaki nimeduwaa nikiwa sina hili wala lile. Nilitamani hata kurudi kijijini lakini kila nikimuwaza Baba niliishiwa na nguvu, kama shangazi amekua mkali vile nilijua Baba angeniua kabisa.
Nikiwa nimenyong’onyea nilimbeba mwanangu, nikachukua na pochi langu na kuanza kurudi nyumbani kwa mume. Nilishakata tamaa na maisha na sikujua ningeenda wapi tena, shangazi alitaka kunisindikiza na gari lake lakini nilikataa, niliondoka na hasira zangu nikiwa nimechanganyikiwa.
*****
UNADHANI ATAONDOKA NA KUMUACHA MTOTO WAKE? ITAENDELEA…
TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU

Tag :
lainnya