Download Mp3 from African

SIMULIZI NDOA YA MAUTI-SEHEMU YA TATU

MSIMLIAJI: Kuluti MC
Maisha yaliendelea na miezi tisa ilifika, sijui niseme kwa bahati mbaya au niseme tu kwa mipango ya Mungu nilijifungua kwa njia ya upasuaji hivyo nilitakiwa kupumzika, lakini nikiwa kitandani nahangaika na mshono kuku walianza kufa mmoja mmoja

Wifi yangu hakua akiwahudumia na kama mnavyojua kuku wakikasa hata wakikaa na uchafu kidogo basi wanakufa wote. Walianza kufa mmoja mmoja na ndani ya wiki moja kuku zaidi ya hamsini walikufa.

Cha ajabu hakuna aliyekua akijali hata mume wangu alikuwa hajali, kitu ambacho kilinistua zaidi kuliko kile cha kuku kufa. Sikujua nini kilikuwa kimembadilisha mume wangu haraka haraka hivyo hasa baada ya mimi kujifungua, nikama alikuw ahataki kujihusisha na mimi kabis awala mtoto.

Taratibu nilianza kusikia maneno kuwa mume wangu alikasirika kwani mtoto hakufanana na yeye na kulikuwa na maneno kuwa mtoto si wake, mimi na mume wangu ni weusi lakini mtoto alizaliwa mweupe. Sikuwa na chakusema lakini ukweli nilikua nikiujua mimi na Mungu wangu.

Nilivumilia ile hali na pamoja na mshono wangu nililazimika kunyanyuka na kuhudumia kuku wa chache wa chotara waliokuwa wamebaki huku nikijipikia na kufua mwenyewe. Nilitamani hata ningekua na mdogo wangu wa kike ningemuita anisaidie kwani hawakua wakinisaidia chochote.

Nakumbuka mara kadhaa kidonda kilifunguka na kutoa dmu lakini nilijikaza hivyo hivyo, ilikuwa nilazima nifanye zile kazi kwani mbali na kuku lakini hata nguo za mtoto nilifua mwenyewe na nisingefanya hivyo angekosa za kuvaa, hata uji nilikuwa nikijipikia mwenyewe.

Kwa kifupi familia nzima ilinitenga na mume wangu alikuwa ni kama adui tu. Kumbuka huo ndiyo ulikuwa uzazi wangu wa kwanza hivyo nilikuwa sijui chochote. Siku pekee ambazo nilikuwa nikipumzika ni zile ambazo shangazi yangu ambaye naye alikua bize sana na kazi zake alikuwa akija kinusalimia.

Hapo hata wao walijifanya kunisaidia kazi na kucheka naye. Yeye ndiyo alikuwa ndugu yangu pekee Dar, wengine walikuwa kijijini, kama ambavyo nilifundishwa uvumilivu katika ndoa sikumuambia chochote na mimi niliigiza furaha.

Maisha yaliendelea lakini hali ilizidi kua ngumu, mume alikua hatoi pesa ya matumizi na kila nikimuuliza alisema pesa si ninazo na hawezi kutoa wakati hajui hata mtoto ni wanani? Sijui alilipata wapi wazo hilo wazo lakini ndiyo ulikuwa kama wimbo mule ndani, yeye na ndugu zake walikuwa wakiongea kimafumbo kuhusu mwanangu.


UNADHANI ATAONDOKA NA KUMUACHA MTOTO WAKE?



ITAENDELEA…


TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU
Tag : lainnya
Back To Top