Download Mp3 from African

SIMULIZI YA KUSISIMUA | MIMBA YA JINI | SEHEMU YA PILI

Msimuliaji Ni KULUTI MC
 SASA ENDELEA...
"Hapana, labda ulitoka eneo la kazi, mgeni alikuwa ofisini kwangu sasa hivi."
"Bosi hakuna mgeni yeyote zaidi ya dada Sara ambaye alikutangulia kuingia kabla yako."
"Mmh! Hebu ngoja."
Mustafa alirudi hadi ofisini na kumuuliza Sara, sekretari wake aliyekuwa bize na kazi kwenye kompyuta.
"Sasa mgeni ametoka?"
"Mgeni gani?" Sara naye alionesha kushtuka.
"Aliyekuwa ofisini kwangu sasa hivi."
"Bosi, hakuna mgeni yeyote aliyefika hapa, kwanza ilianza lini kumruhusu mgeni aingie ofisini kwako bila ruhusa yako?"
"Sasa huyu mgeni kaingiaje na kapitia wapi?"
"Bosi mgeni unayemsema umemuona wapi?"
"Hebu njoo ofisini."
Sara na Mustafa waliongozana hadi ofisini ambako bado harufu ya manukato makali ilikuwa ikinukia.
"Bosi pafyumu nzuri kama hii umeitoa wapi?" Sara alisema huku akinyanyua pua zake kuivuta.
"Sara, haya manukato nimeyakuta baada ya kurudi kutoka msalani."
"Muongo!" Sara alishangaa.
"Kweli kabisa, yanaonekana ya huyo mgeni aliyeingia ofisini."
"Sasa kapitia wapi?"
"Hebu subiri."
Mustafa alisema huku akichukua simu yake juu ya meza, aliangalia namba iliyoingia yenye jina la Shehna na kuipiga. Simu ilionekana ipo bize inazungumza.
"Simu yake inaongea."
"Mmh! Si ulitoka nje, mlinzi anasema kuna mgeni aliingia?"
"Hata yeye anasema hajamuona."
"Mmh! Mtu gani tusimuone wote basi atakuwa jini."
"Hapana si jini, nitampigia tena."
Mustafa aliachana na mambo ya mgeni asiyeonekana, alikumbuka amesahau pete yake msalani kumuwahi mgeni. Alikwenda hadi sehemu ya kunawia mkono, alishtuka kukutana tena na harufu ya manukato aliyokutana nayo ofisini kwake. Lakini alipoangalia juu ya sinki hakuiona pete yake.
Alishtuka na kuangalia chini labda imeanguka vilevile hakuiona, aliingia msalani kuitafuta pia huko hakuiona. Akili yake ilimweleza kuwa pete ile iliivua wakati akitaka kunawa mikono. Alitoka hadi kwa Sara kumuulizia.
"Sara kuna mtu kaingia msalani wakati naingia ofisini?"
"Hakuna."
"Unajua wakati nanawa niliweka pete yangu ya ndoa juu ya sinki, baada ya kuzungumza na simu niliwahi ofisini lakini ajabu nimerudi sijaikuta."
"Mmh! Umeangalia vizuri?"
"Nimeangalia, au Sara, leo sikuja na pete?"
"Umekuja nayo, si unakumbuka nilikutania siku ukiipoteza utamwambia nini mkeo."
"Nakumbuka, sasa imekwenda wapi?"
"Mmh! Mbona leo mauzauza."
"Huwezi kuamini ile harufu ya manukato nimekutana nayo tena msalani."
"Wewe!" Sara alishangaa.
"Kweli Sara."
"Bosi, hebu tulia kwanza inawezekana leo umeamka na mawazo mengi kutokana na ishu ya wifi. Nilikueleza mkienda Mbagala kila kitu kitakuwa sawa, yule mama kawasaidia wengi. Sema bosi tatizo ulilificha sasa hivi ungekuwa na mtoto."
"Ni kweli, jana niliporudi nimemkuta wifi yako analia."
"Tatizo?"
"Lile lile la mtoto, anasema sijui kawasikia watu wakimsema kwa mafumbo kwamba tasa."
"Hukumweleza tuliyozungumza jana?"
"Nimemweleza lakini anasema amechoka na uongo wa waganga, toka tuanze kuhangaikia mtoto huu mwaka wa tano sasa."
"Mwaka wa tano?" Sara alishtuka.
"Ndiyo, na fedha tuliyopoteza tungeweza kujenga nyumba kubwa na gari mbili."
"Bosi yule mama kiboko wapo waliokata tamaa kama yeye lakini walipotumia dawa zake walipata watoto."
"Mbona kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa hivyo hivyo mpaka waliopata watoto tuliwaona, lakini alipotumia hakupata kitu."
"Hebu nendeni Mbagala tuone."
"Alikubali kwa shingo upande, hivi namsubiri amesema atanipitia saa tano tuelekee huko mbagala."
"Basi bosi kapumzishe akili utajua pete umeiweka wapi."
Mustafa alirudi ofisini kwake na kukaa kitini, alijitazama vidole vyake asiamini kama kweli hakuja na pete. Akiwa bado anavishangaa vidole vyake simu yake iliita, alipoangalia alikuta ni Shehna. Aliipokea:ITAENDELEA.............!!! TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU
Tag : lainnya
Back To Top