Kundi nzima la Amahunja Music kutoka mkoani Gitega, inazidi kukubalika pande nne za Republic of Burundi kwa vibao vyoa kama Koreta, Ndimubandi, Njera.
Amahunja Music ilirikodi nyimbo mbili ( Njera na Ndimubandi) huku ikifanikisha kushirikiana na wasanii wengi nchini kama Amibaso (Igipoli kizira igiturire), Musebo (Mpa ibikorwa), Jeune Poli ( Mpinkwano zanje) huku wakifanikisha ku shoot video mbili (Koreta na Ibijumbu) na demo tatu.
Kundi hii inayotamba na kibao chao Njera, walifunguka kwa kile ambacho kinazidi leta utata kwenye game ya muziki wa Republic of Burundi Flava na kusema kuwa kinawauma sana kuona wasanii wa Republic of Burundi wakifanya demo ya bei chini sana tofauti na wasanii wa nje wakija nchini. Waliongeza nakusema kuwa labda wa promota wana promote mziki wa nje zaidi, labda warundi hawajatambua faida ya kazi zao. Kundi hii imezidi kusema kuwa mpaka sasa hakuna hakimiliki na ndio sababu ya wimbo wao kuibiwa na wakabadilisha jina la Koreta na kutumia jina la Jeanine jambo ambalo liliwakera sana na kukosa la kufanya.
Tuwakumbushe kuwa kundi la Amahunja Music iko kwenye arakati ya kuandaa albamu mwaka ujao pia kunakijana ajulikanaye kama Mr Khalid ndie anaye zidi kuwasaidia kutunga nyimbo na video.
Amahunja Music liliitaka gazeti la Mishe Mishe kama inawezekana kuleta Radio au TV ambayo ina lengo la kutangaza kazi za wasanii kwasababu ni gazeti linalo fatiliwa na watu wengi Afrika Mashariki.
Aidha, mwaka ujao wa 2017 kundi hili lilihaidi mashabiki zawo kufanya kazi ya ziada tofauti na mwaka 2016 ili wafanikishe lengo la kujitangaza kimataifa zaidi.