Download Mp3 from African

Mwenyekiti almanusra kutumbuliwa kwa ubadhilifu na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero

Katika kile  kinachohisiwa ni ubadhirifu wa fedha  za uma  mwenyekiti  wa  kijiji cha madizini ,kata ya Turiani  wilaya ya mvomero  khalifa Ahmed almanusra atumbuliwe na mkuu wa wilaya hiyo muhamed Italy ,mbele ya mkutano wawananchi wa kijiji hicho kwa kushindwa kutoa  maelezo wapi ziliko fedha  shilingi 1,500000,zilizotolewa na mbunge wa  jimbo hilo zikiwa ni kwaajili ya ujenzi WA madarasa na vibali vya makaburi.

Wakitoa malalamiko mbele ya mkuu wa wilaya kuhusu MWENYEKITI huyo mwananchi hao wamesema  kuwa MWENYEKITI huyo ameshindwa kutoka ufafanuzi wawapi ziliko fedha  hizo na mala kadhaa amekuwa akiwatishia baadhi ya mwananchi walikuwa wakihoji kupitia vikao vya kusoma mapato na matumiziya kijiji hicho jambo ambalo  waliamua kulipeleka kwa afisa  mtendaji wa kata  hiyo.

Akitoa ufafanuzi mbele ya mkuu wa wilaya juu ya sakata hilo mtendaji wa  kata abdalla maganza amesema ni kweli amepokea malalamiko hayo kutoka kwa wanakiji hao naye akaitisha kikao cha uongozi wa  kijiji ili kuweza kupata ufafanuzi WA jambo hilo  na baada ya kushindwa kupata ufafanuzi wa kutosha akaamua kulifikisha jambo hilo polisi na polisi wamerfikisha mahakamani jambo hilo ili liweze kutatuliwa kisheria.

 Akitoa mamuzi mbele ya mwananchi waliokusanyika kwenye mkutano huo mkuu wa  wilaya amemuagiza mkurugenzi wa  halmashauri hiyo florent  kyombo  kuhakikisha anamtuma mkaguzi wa ndani aende kukagua mapato na matumizi ndani ya kijiji hicho na majibu yapatikane ndani ya wiki mbili na kama kuna ubadhirifu WA fedha  hata za kisheria zichukuliwe kwa mtuhumiwa ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Ziara hizi ni muendezo kwa utaratibu ambao mkuu wa  wilaya hiyo aliojiwekea kuhakikisha yeye na mkurugenzi  na wakuu WA idara  wanatembelea vijiji vyote vya wilaya hiyo ili kutatua kero zinazowakabili mwananchi na kuweza kuzitatua.
Tag : lainnya
Back To Top