MSIMLIAJI: Kuluti MC
“Dada huyo ni mume wako kweli?” Aliniuliza kijana mmoja ambaye alikuwa pale dukani.
Nilimuangalia kwa wasiwasi nikataka kudanganya niseme labda ni bosi wangu lakini nilikumbuka wakati ananitukana alisema “Najuta kuoa mwanamke mbinafsi kama wewe! Unawatesa sana ndugu zangu!”
Nilitaka pia kutokumjibu kwani yalikua hayanihusu lakini alikuwa amenunua vitu vingi na kwa muonekano wake angekuwa ni mteja wa kudumu.
“Ni mume wangu ndiyo” Nilimjibu kwa kifupi huku nikijifanya niko bize kumuandikia risiti, sikutaka aendelee kunichunguza. Aliniangalia kwa huruma huku akitingisha kichwa kusikitika.
“Wanawake mnavumilia mengi sana...” Aliongea kwa masikitiko huku akipokea risiti niliyokuwa nikimkabidhi. Tayari vijana wangu walishamaliza kupakia mizigo aliyokua amenunua kwenye gari aliyokuja nayo aina ya Toyota Double Cabin.
Aliwakabidhi hela ya kupakia kisha akaingia kwenye gari na kuondoka zake. Nilimuangalia akati anaondoka huku nikimshukuru Mungu uwepo wake pale kwani nina uhakika kama asingekuwepo basi siku ile ningechezea makofi. Mume wnagu aliona aibu kunipiga mbele ya mwanaume mwenzake tena akiw ahamfahamu.
*****
Siku yangu ilianza kuharibika asubuhi, wakati nimeenda kuchukua vifaranga nilimuacha wifi na mfanyakazi pale dukani, niliporudi sikumkuta wifi yangu na nilipomuuliza mfanyakazi aliniambia aliondoka pale tu nilipoondoka na kusema anaenda Kariakoo.
Sikuwaza sana kwani ilikua ni kawaida yake allikua akifanya kazi anavyojitakia. Nilikasirika pale alipokuja Mama John mteja wangu mkubwa, nilimuambia mfanyakazi wangu kumpa shilingi laki tatu nilizokuwa nimemuachia asubuhi wakati naondoka ili Mama John akija kama sijarudi ampe.
“Dada amezichukua, amesema kuna vitu anaenda kununua mjini..!” Alinijibu akimaanisha wifi yangu kazichukua zile pesa. Hasira zilinipanda kwani wakati ule sikua na hata shilingi mfukoni, hela zote nilinunulia mzigo na Mama John ni mteja wangu wa muda mrefu, ilinilazimu kukopa kwa jirani na kumkabidhi huku nikijifanya hakuna kitu kibaya kilichotokea.
Haikupita nusu saa wifi yangu alirejea, hata kabla sijamsemesha alitoa maronja ronya ya nguo aliyonunua huko mjini na kuanza kumuonyesha mfanyakazi na wa mama wengine. Nilijua alikua anafanya makusudi ili niongee hivyo nilimuangalia tu bila kusema chochote.
Sikutaka watu wajue nimekasirika hivyo alipomaliza na kuingia dukani bila kusema chochote nilitulia mpaka mfanyakazi alipotoka ndipo kistaarabu nilipomuuliza mbona amechukua pesa za mteja wakati akijua hatuna pesa, pesa yote tulienda kununulia mzigo, angalau hata ungeniambia nijue chakufanya.
Aliniangalia kwa dharau kisha akasema.
“Kwani pesa ni zakwako, hizi mali ni za Kaka yangu na yeye nilimuambia akaniambia nichukue..”
“Hata kama lakini ungeniambia na mimi…”
“Bibieee! Nikuambie wewe ili? Hizo zote unazopeleka kwenu unatuambia? Mfyuuuu! atomic seat out 79 unafikiri hatujui?”
Alisonya kwa nguvu, nilinyamaza tu bila kusema chochote. Ukimya kidogo ulitawala, nikama alitaka niongeee lakini sikunyanyua tena mdomo wangu, alianza kuongea maneno yake ya kashifa, kusema sema na kusengenya lakini sikujibu chochote. Kuona vile alichukua nguo zake na kuondoka bila hata kuaga.
Jioni sasa baada ya mume wangu kutoka kazini ndiyo akaja pale, kakunja ndita na mihasira yake akisema ninamnyanyasia ndugu zake. Alinitukana matusi ya nguoni mbele ya wafanyakazi na wateja, nilimsikiliza bila kumjibu kwani nilijua nikinyanyua tu mdomo ni kipigo.
Hilo nalo lilikua kosa kuwa nina kiburi simjibu, simuongeleshi nina dharau na mambo kama hayo. Hata hivyo sikuongea, nilibaki tu kimya mpaka akaona kama anajichora akaondoka.
*****
UNADHANI NINI KIMETOKEA?
ITAENDELEA….
TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU

Tag :
lainnya