MSIMLIAJI: Kuluti MC
Maisha yetu hayakuwa hivyo, baada ndoa maisha yetu yalikuwa mazuri, wakati huo ndiyo nilikuwa nimemaliza kidoto cha sita, sikufaulu vizuri hivyo nilibaki nyumbani kwa kama miezi sita ndipo nilipoolewa na mume wangu ambaye alikuwa ni mhasibu.
Erick alikuwa akiishi nyumbani kwao, kama mtoto wa kwanza alichukua jukumu la kulea familia yao baada ya Baba yake kufariki. Alikuwa akiishi yeye Mama yake na wadogo zake wanne wawili wakike na wawili wakiume.
Mwanzoni mambo yalikua mazuri kidogo, Mama mkwe na wifi zangu ambao walikuwa wakubwa kidogo walinipenda, shemeji zangu walikuwa wadogo hivyo walikuwa wakiniheshimu na mpaka sasa wananiheshimu.
Lakini hali ya mule ndani haikunifurahisha, kila kitu tulikuwa tukimtegemea mume wangu na kama unavyojua mishahara ya serikali haitoshi.
Yaani mimi, Mama mkwe ambaye hakuwa mzee sana, wifii yangu mkubwa ambaye alikuwa ameacha shule kidato cha tatu baada ya kupewa ujauzito na kutelekezwa na mwanae, wifi yangu mwingine ambaye alikuwa kidato cha nne na shemeji zangu wawili ambao mmoja alikuwa kidato cha kwanza na mwingine darasa la sita, tulikuwa ni kula na kulala tu.
Nilimuonea huruma mume wangu ndipo nilimpomuomba mtaji wa kufanyia biashara, hapo ndipo mambo yalipoanza kuharibika. Alinipa mtaji wa shilingi laki moja (kipindi hicho laki moja ilikua hela nyingi kidogo) na nikaanza kuuza mayai ya kisasa kwa bei ya jumla na rejareja.
Nilitaka kufanya biashara ya mayai nikiwa na lengo la kufuga kuku kwani kabla ya kuolewa nilikuwa nikiishi na shangazi yangu (ndiye aliyenileta Dar)ambaye alikuwa akifuga kuku na niliona kiasi cha fedha alichokuwa akiingiza hivyo kutamani kufanya ile biashara kwani nilishapata kauzoefu kidogo.
Wakati huo huo nilijenga banda dogo la kuku pale nyumbani kwani kulikuwa na uwanja mkubwa na kuanza kufuga kuku wa mayai. Kila kitu nilikuwa nikifanya mwenyewe si Mama mkwe wala wifi zangu walionisaidia ingawa Mama mkwe na wifi mkubwa walikuwa tu pale nyumbani.
Wakati huo nilikuwa na ujauzito wa mtoto wangu wa kwanza. Baada ya kuanza biashara na kuanza kuingiza vipesa kidogo mambo yalibadilika, mwanzoni kazi za nyumbani tulikuwa tukisaidiana ila baada ya kuanza biashara kazi zote walikuwa wakiniachia mimi.
Sikuongea lakini kila siku Mama mkwe alikuwa akiongea kuwa kazi ya mwanamke ni kumhudumia mume wake, alikuwa akiongea kwa mafumbo na mara kadhaa alimuonya mume wangu kuwa huyu mwanamke atakuja kukutawala akipata pesa.
Mwanzoni mume wangu alikuwa akipuuzia kwani kufanya kwangu kazi kulikuwa kukimpa unafuu wa maisha, angalau sasa aliweza kununua shati jingine kwani kusema kweli faida ilikuwa kubwa na namna nilivyokuwa na weza kuongea na wateja basi ilisaidia.
Pia shangazi yangu ambaye alikuwa mfanyabishara mkubwa lainiunganisha na baadhi ya wateja wake na mara kadhaa alikuwa akinikopesha mzigo mkubwa. Nilipata pesa na kujenga mabanda mawili makubwa na kuanza kufuga na kuku wa nyama.
Kazi zilinizidi ukichanganya na ujauzito ambao nilikuwa nakaribia kujifungua pamoja na ugumu wa kuhudumia kuku nilikuwa nahitaji msaidizi, nilimuomba wifi yangu anisaidie katika kuhudumia lakini alikataa akisema siwezi kumtumikisha kama mfanyakazi.
Niliongea na mume wangu ambaye alimlazimisha kufanya ile kazi kwani hakua akifanya kazi yoyote wakati alikua akila bure yeye na mwanae. Hilo lilizua balaa kubwa kwa Mama mkwe akisema nimemtawala mtoto wake namuendesha.
Maneno yalikuwa mengi kwakweli lakini nilivumilia kwani mume wangu alikuwa upande wangu, kila wakati aliniambia kuwapuuza tu. Na mimi nilimsikiliza hivyo niliyasikiliza maneno yao na kuyapuzia.
*****
UNADHANI ATAONDOKA NA KUMUACHA MTOTO WAKE?
ITAENDELEA…
TUNAPATIKANA KWA SIMU NO; +25571490303/ Whatsapp HII NAMBA NI KWAAJILI YA USHAULI AU MAONI YUU YA SIMULIZI ZETU

Tag :
lainnya