Download Mp3 from African

STORY YA KWELI PENZI LA MKE WA BOSI. SEHEMU YA KWANZA.

MSIMLIAJI: Kuluti MC
Naomba nianze kwa kusema umasikini mbaya sana, kwani isingekua umasikini nisingefanya haya yote. Baada ya kuishi kwa maisha ya kubangaiza sana huko jijini Mbeya ndipo siku moja nilikutana na mzee mmoja akiwa anahangaika kulisukuma gari lake ambalo lilikua limegoma kuwaka aliponiona akaniita na kuniomba msaada wa kumpush kidogo.
Kama kawaida sikukataa nikampush had gari ilipowaka basi akaniita ndani ya gari na kuniuliza nilikua naelekea wapi nikakosa cha kumjibu kwani nilikua sina mwelekeo zaidi ya kuzurula nikamsimulia jinsi ninavyohangaika na kuteseka na maisha ndipo akaniahid kunisaidia na kuniomba niende naye nyumbani kwake na nikaishi naye huko kwani ana familia yenye uwezo mkubwa tuu.
Sikua na jinsi zaidi ya kukubali maana nilikua nimechapika haswaa na maisha ya mtaani tulitoka pale hadi nyumbani kwake hakika jumba lilikua kubwa na la kifahari tukaingia ndani akapack gari tukashuka akanikaribisha ndani nikaingia wakat naingia nikamwona mama mmoja mnene mweupe amekaa kwenye sofa huku sehemu kubwa ya mapaja yake yakiwa nje. "Karibuni" Alisema yule mama huku akiangalia kwa jicho la matamanio Ahsante mumewe aliitikia na kumwambia nimekuja na mgeni atajitambulisha yeye mwenyewe,
Basi nikakaa pale na kuanza kujitambulisha Mimi naitwa Yusuph Ng'ahala ni mzaliwa wa hapahapa Mbeya sina wazazi wala sina ndugu na sifahamu chochote kuhusu wazazi wala ndugu. Yule mama akanitizama na kusema pole mwanangu usijali kuanzia sasa sisi ndio wazazi wako na ni ndugu zako akawa ananipa mkono huku akisema karibu nilimpa mkono yule mama lakini nikawa nashangaa anitekenya kwa vidole viwili sehemu ya viganja vyangu huku akisema karibu sana mwanangu jisikie uko nyumbani nami nikaitikia kwa kusema ahsante huku nikiuvuta mkono wangu na kurudi kukaa katika ile sofa.
Basi mzee yule akasema huyo ni mama mwenye nyumba hapa kuna wadogo zako wameenda shule utawaona badae kwa sasa ngoja nikuonyeshe chumba cha kulala alafu kesho ntakuelekeza kazi za kufanya hapa nyumbani sawa eee?? nikajibu sawa mzee wangu basi akanipeleka chumba ambacho kilikua nje ya lile jumba na kuniambia utakua unalala humu chumba kilikua kimekamilika basi nikaingia mle ndani na kukagua kagua na kujiridhisha.
Kwa kua nlikua mgeni sikua na la kufanya nikaamua kuuliza bafu lilipo na kuingia kuoga na kurudi kulala. nililala usingizi nikaja kushtuka mida ya saa 12 jioni ambapo mama alikua akiniita na kusema niende sebuleni nikaamka na kuelekea sebuleni nikafika na kuwakuta watoto wa kike watatu na wa kiume mmoja wote wakanisalimia nami nikaitikia huku nikiketi basi mama akasema hawa ni wadogo zako huyo anaitwa Happy yuko cast three, na huyo ni Jane yeye yuko cast five na huyo anaitwa Zuwena yuko cast i na huyo mdogo anaitwa Samweli yeye yuko darasa la sita. mama akawageukia wanawe na kusema huyu ni kaka yenu tutakua naye hapa mmuheshim sana wakaitikia na akawambia haya kabadilisheni nguo za shule alaf mmsaidie dada kupika sawa eee basi wale watoto wakaondoka wote na kuelekea vyumbani mwao nami nikabaki na yule mama pale sebuleni.
..ITAENDELEA SEHEMU YA PILI ..
Tag : lainnya
Back To Top