| Mwanzilishi wa Divine Worship Joshua Ngoy Ngoy ama wengine wanavyomfahamu kama Joshua music kama anavyoonekana hapo pichani . |
Na.Veo Ignatus Arusha/Kilimanjaro
Divine Worship imejiandaa kutembelea kituo cha watoto yatima na wajane kilichopo Manispaa ya Moshi mjini Mkoani Kilimanjaro kiulikanacho kama Kitaa Hope Children Home wakiwa na lengo la kuwatembelea na kuzifahamu changamoto mbalimbali wanazopitia watoto hao pamoja na wakina mama hao wajane .
Hayo yamesemwa na mwanzilishi wa kundi la Divine Worship Joshua NgoyNgoy ambapo amesema kuwa wameamua kutenga siku maalumu kukitembelea kituo hicho ili kuwaonyesha upendo kwa watoto hao, ili na wao wajisikie ni binadamu wengine"tutakaa nao,tutakula nao pamoja ikiwezekana hata kucheza nao kwa pamoja ili na wao wajisikie faraja na kuwa jamii inawakumbuka pia"
Aidha amesema kuwa hawa watoto yatima na wao wanahitaji kujisikia vizuri kama watu wengine wanavyojisikia.
"Yatima hawa na wajane wanatamani na wao wawe na maisha mazuri kama yale unayoishi wewe hivyo basi tuungane kwa pamoja kwenda kuwatembelea watoto hawa ,ukiwa na chakula ,mavazi,,pesa kiasi chochote tuungane kwa pamoja tukawatembelee naomba sapoti yenu kukitembelea kituo hichi,kwani jambo kama hili tukifanya kwa moyo linampa Mungu utukufu" alisema Joshua.
Amesema siku ambayo wameitenga ni tarehe eighteen februari ambapo itakuwa siku ya jumamosi saa nne asubuhi, hivyo amewaomba watanzania wote ,makampuni mbalimbali pamoja na wadau mabalimbali ili kuwasaidia watoto hawa pamoja na wajane waliopo kituoni hapo.
Tag :
lainnya
