Label kubwa ya muziki iitwayo Instincts Records itazinduliwa Jumamosi hii jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo utafanyika kwenye hoteli ya Regency Park iliyopo Mikocheni.
“Lengo la launch ya kesho ni kujumuika pamoja na wadau kwenye tasnia, kufahamiana vizuri na kujenga umoja na ushirikiano pamoja na kuitambulisha squad nzima,” afisa uhusiano na msemaji wa label hiyo, Raheem Da Prince ameiambia Bongo5.
“Pia itatambulishwa kazi ya msanii mpya aliyesainiwa Insticts anaitwa Shose, runway na Video iliyofanywa na Hanscana itaonyeshwa mpango mzima ukisindikizwa na Dj Mkali International Dj Vasley,” ameongeza.
“Lengo la Insticts ni kukuza vipaji na kuipeleka tasnia ya muziki wa kizazi kipya kwenye levo za kimataisha hapa tunazungumzia Bad Boys ent sort of thing.”
“Kwa mashabiki wanaopenda kuwepo mlangoni wataacha elfu ishirini. Kuanzia saa 1 jioni Regency Park Hotel Mikocheni
Tag :
lainnya