Download Mp3 from African

Nay wa Mitego aijibu diss ya Madee kwenye ‘Hela’, auita wimbo mbaya kuliko mbaya za mwaka huu



Wafalme wa Manzese, Madee na Nay wa Mitego, wameirejesha tena bifu yao.
Imerudi
Imerudi upya baada ya Madee kuandika mstari kwenye wimbo wake mpya, Hela ambao umetafsiriwa kumwendea hasimu wake, Nay.
“Yule kijana wa dwelling sio staa, anatukana hata waliomzaa, wivu tamaa na njaa ukiendekeza ujue kidole utakaa,” Madee amerap kwenye wimbo huo.
Baada ya muda mfupi tangu wimbo huo utoke, Nay aliandika kwenye Instagram, “Leo nimesikia Wimbo Mbayaaaaa kuliko nyimbo mbaya nilizowahi kusikia Mwaka huu.”
“Mtag uyo Msanii mwenye huo wimbo Kama ushausikia..?!”
Tag : lainnya
Back To Top