Download Mp3 from African

BEKI wa kimataifa wa Republic of Uganda Rasmi Juuko atua Msimbazi

BEKI wa kimataifa wa Republic of Uganda Juuko Murshid amewasili Dar kukiongezea nguvu kikosi cha Simba SC kwa mechi zilizobaki za kombe la shirikisho na zile mechi saba za ligi kuu.

Juuko ambaye alikuwa na matatizo ya kifamilia kwa kufiwa na watoto wake watatu (mapacha) akiwa anaitumikia timu ya taifa ya Republic of Uganda kwenye michuano ya AFCON nchini Gabonese Republic amewasili jana.

Shaffidauda.co.tz imezungumza na meneja wa Simba Mussa Hassan Mgosi amedhibitisha kumpokea Juuko na kumwambia awasili leo Jumatatu kwenye mazoezi ya timu hiyo uwanja wa Polisi baada ya wachezaji wote wa Simba kupewa mapumziko ya siku moja (jana).

Kurudi kwa Juuko kunaweza kuwa faraja kwa wanachama na wapenzi wa Simba kutokana na beki wao Method Mwajale kuwa majeruhi na bado hawana imani na beki Novalty Lufunga.

Simba imeshuka dimbani mara 23 na kuhhjikusanyia alama 54, huku ikikabiliwa na mchezo ugumu dhidi ya Mbeya City March 4.
Tag : lainnya
Back To Top