Download Mp3 from African

Kama mbaya iwe mbaya tayari amelianzisha yeye ila nitapambana_Akes Don

Msanii wa muziki wa Burundifleva Akes Don alifunguka Februari 28 kwenye Radio Culture katika kipindi maarufu nchini Republic of Burundi kikifahamika kwajina la Stay Tune on Sanaa kikiongozwa na watangazaji mahiri  Peniel na Douglas, na kusema kuwa wasanii waliotangulia wanauoga na wasanii chipukizi (upcoming) ndio maana kila siku wanazua mambo mabaya ya  kutaka kuwazimisha kwenye game ili wabaki pekee yao kitu ambacho Akes amesema hakiwezekani hata kidogo na kama mbaya iwe mbaya.

Alipoulizwa na shabiki kwenye kipindi kama anabifu na msanii wowote na endapo bifu hiyo hipo basi afunguke kisa cha mgogoro wake na msanii Sat B ambae kwasasa anajiita Tiger.

watu wanafikiri kama nina bifu na msanii Saturday B ila watambue kuwa sina bifu na msanii, sometimes wasanii waliotutangulia wanakuaga na uoga na wasanii chipukizi (upcoming), katika muziki usiokopi  yule aliyekutangulia ila muogope yule aliye nyuma yako. Levo ya wasanii wa Republic of Burundi naitambua siwezi poteza mda wangu kutengeneza bifu wakati uwezo wetu hauturuhusu kufanya bifu labda nifanye na msanii  wa nje ambae atakaenifikisha mbali . Alisema Akes Don

Aidha, mashabiki wanataka kuona wasanii hawo wawili wakishirikiana pamoja na kufanikisha kutoa wimbo wakiwa pamoja, Akes Don alisema kwamba hana mpango wowote wala hajawahi kufikiria kitu hicho labda siku za mbele huku akiongeza kuwa ana kazi nyingi zipo studio na ameshirikiana na wasanii wa nje.

Tuwakumbushe kuwa msanii Akes Don ambae Machi 04, atazindua video ya wimbo wake Kizunguzungu, alisema msanii anayekubali sana nchini Burundi, ni Yoya Jamal na Big Fizzo na kusema kwamba hajawai kuona kazi mbovu ya wasani hawo wawili.


 

Back To Top