Download Mp3 from African

Mama yake Masau Bwire anahitaji faraja kutoka Ruvu Shooting

Leo katika uwanja wa Mabatini, Mlandizi, Kibaha, Pwani, Ruvu Shooting anamualika Tanzania Prisons katika mchezo wa VPL.

Ushindi kwa Ruvu Shooting ni muhimu sana kwa timu ili ijiweke katika nafasi ya juu kimsimamo.
Lakini pia ni muhimu sana na faraja kubwa sana kwa Mama yangu mzazi Nyakwesi Mabamba Bwire ambaye ni mgonjwa.

Jana nikiwa naye Kijijini Mwiruruma, Musoma, pamoja na kuugulia maumivu makubwa ya maradhi yanayomsibu, aliniuliza maendeleo ya Ruvu Shooting na kuitakia mafanikio.

Vijana, wachezaji wa Ruvu Shooting, ambao nawaamini sana kwa ubora wa kucheza mpira, ebu leteni faraja kwa Mama yangu mzazi, mtu mzima sana aliyezaliwa mwaka 1931 kwa kupata ushindi dhidi ya Tanzania Prisons hii leo, Mabatini.
Tag : lainnya
Back To Top