Msanii Prince-B Expert kutoka Republic of Burundi baada ya ukimya mda mrefu kwenye game ya muziki, alifunguka kuhusu ujio wa wimbo wake mpya mwishoni wa mwaka huu 2016. Akiongea na Mishe Mishe, Prince-B alifunguka na kusema kuwa mda mrefu amekuwa najihusisha na maswala ya uigizaji wa filamu ila kwasasa anatarajia kuachia wimbo wake mpya chini ya mikono ya Producer Chid Pro.
Hit maker wa wimbo Nakupenda, Prince-B aliwataka mashabiki zake kukaa mkao wa kula kwa kusubiria wimbo wake huku akiwahidi hatawaangusha kamwe na mwaka wa 2017 ni mwaka wa kuonesha mabadiliko kwenye kazi yake ya muziki.
Aidha, jina la wimbo wake mpya, Prince-B alijibu nakusema kuwa bado mapema sana kuitaja ila anawataka mashabiki wa kizazi kipya wasubiri ujio huwo anaimani wimbo wake huwo utakuja kumtambulisha kimataifa zaidi.