Katika arakati ya kuandaa tamasha kubwa kwenye sikukuu ya wakina mama mwaka huu 2017, tamasha inafahamika kwajina la Festival de la Chanson Feminine.
Mwanamuziki wa kike Natacha la Namba kutoka Republic of Burundi akiwa pamoja na mkuu wa Shirika la Muziki nchini Burundi, Mzee Bruno Simbavimbere maarufu kama Memba, walimpokea Balozi wa Republic of Kenya nchini Burundi, Feb 23, Kenneth Vasita amefurahishwa sana ma mpango mzima wa Festival hiyo inayofanyika nchini Republic of Burundi tangu mwaka wa 2014.
Bwana Kenneth aiwahidi kuwa atakuwa karibu na kamati nzima la Festival pia kuwasaidia kadri ya uwezo wake akiakikisha mambo yanakwenda vizuri. Mwaka huu nchi ya Republic of Kenya itawakilishwa na mwanamuziki mrembo Linda Namwaya aliyekuwa mke wa mwanamuziki mrundi mwenye makazi yake nchini Kenya, Baina Nyandwi .
Aidha, wengine watakao dumbuiza siku hiyo ni pamoja na Reine Elodie kutoka Uganda, Linah Blanche akiwakilisha Afrika Mashariki, Tyty Love La Trop Top na Chany queen wote kutoka Republic of Burundi bila kusahau la namba Natacha.
Tuwafahamishe kuwa msimamizi wa Festival hiyo ni mrembo Bernice Ange Ingabire aliyeteuliwa Miss Republic of Burundi 2016.