Hit maker wa wimbo "Maisha na Muziki" Dj Pro alifungukia African Mishe na kusema kuwa hakuna watu wengine wanao rudisha nyuma na kuua soko la muziki la Republic of Burundi Flava kama wandaaji wa ma demo nchini.
Aliyasema hayo baada ya kuwekwa kwenye bango la demo moja bila idhini yake huku akiumizwa na kitendo icho na kupeleka malalamiko yake kwenye makao makuu ya shirika inayousika na music nchini Burundi "AMICAL". Msanii huyu ameiomba AMICAL iwasiliane na wandaaji wa demo nchini ili jambo hii isijitokeze tena kwasababu imekua sugu nchini Burundi.
Alipoulizwa yapi madhara ya kumuweka msanii kwenye bango bila kuwasiliana na wausika wa msanii?
Msanii Dj Pro alijibu na kusema kuwa
"wandaaji wa demo nchini wanaandaa kwa maslahi yao ilimradi wapate watu wengi kwenye demo yao kupitia jina la msanii wakati hawajaozungumza kitu chochote na msanii mwenyewe, wakisahau kama wanaharibu soko la muziki la Republic of Burundi Flava kwasababu nitakapo andaa demo yangu sitopata mashabiki, watafikiri labda mchezo ni uleule".