Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwasili mahakamani leo pamoja na mahabusu wengine leo 4januari2017 .Picha na Vero Ignatus Blog.
Wakili anayemtetea Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,John Mallya akiwa anazungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama leo 4Januari 2017.Picha na Vero Ignatus Blog |
Mke wa mbunge wa Arusha mjini Neema Lema akiwa nje ya mahakama kuu kanda ya Arusha leo 4januari 2017.Picha na Vero Ignatus Blog.
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwapungia watu waliokuwapo mahakamani tayari kwa kurudi mahabusu leo 4januari2017 .Picha na Vero Ignatus blog.
Na.Vero Ignatus ,Arusha
Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjinia melazimika kurudishwa tena rumande mara baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kushindwa kutoa uamuzi baada ya upande wa Jamhuri kukata rufaa kwenda Mahakama ya Rufani kupinga mbunge huyo kupewa dhamana.
Jaji wa Mahakama kuu ya Arusha aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Salma Magimbi ameshindwa kutoa maamuzi kutokana na upande wa Jamhuri kukata rufaa ya mahakama kuu ya Rufaa kupinga dhamana dhidi ya Lema.
Jaji huyo amesema hana mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kutokana na uamuzi huo; hivyo kusababisha mbunge Lema kurudishwa tena rumande.
Kwa upande wa Wakili mtetezi wa Mbunge Lema John Mallya akielezea mwenendo wa kesi hiyo kwa niaba ya mawakili wenzake amesema wamesikitishwa na uamuzi u
Amesema jambo hilo linalobishaniwa na upande wa Jamhuri lipo wazi na kwamba wanajipanga kwenda katika mahakama kuu ya rufaa kabla yao ili shauri hilo liweze kusikilizwa na mteja wao amekubaliana nao.
Mbunge huyo amerudishwa tena Rumande hadi hapo kesi hiyo itakaposikilizwa tena ambapo mpaka sasa amefikisha siku 61 akiwa mahabusu
Tag :
lainnya