Muimbaji wa Komela, Dayna Nyange amesema atamuonesha wazi mpenzi wake baada ya kuolewa.
‘Nilishasema kuwa ntaweka mahusiano yangu hadharani ya mume wangu sio mpenzi au mtu tu ambaye niko naye kwasababu sisi ni binadamu yanatokea mengi pia ujana yanatokea mengi. Unaweza kuwa na mtu ambaye unampenda sana lakini huwezi kujua ndani ya moyo wake na yeye anakupenda the same au sio,” alisema.
“Mmeonekana siku mbili tatu yanatokea majaribu hamko wote, tena kesho upo na mahusiano mengine unayaweka mnapishana hamko wote, kinakuwa sio kitu kizuri,” amesisitiza.
Tag :
lainnya