Download Mp3 from African

Msanii Ben Pol awashangaa watu elfu mbili kudai hawaupendi wimbo ‘Muziki’ wa Darassa

Msanii wa muziki wa R&B Ben Pol amewashangaa watu elfu mbili kutupia mtandao wa video YouTube kudai hawaupendi wimbo ‘Muziki’ wa Darassa ambayo bado unaendelea kufanya vizuri katika sehemu mbalimbali za Tanzania na nje.

Katika mtandao huo wa video kuna sehemu mbili ambazo humwezesha shabiki wa muziki kuclick kama anaipenda kazi hiyo au haipendi.
Katika video ya Darassa ya wimbo Muziki watu elfu mbili ameonyesha hawaupendi wimbo huo baada ya kuclick sehemu ya dislike.
B
Muimbaji huyo ambaye ameshiriki katika wimbo huo baada ya kuona tukio hilo alionyesha kushangazwa kutokana na wimbo huo kufanya vizuri sana.
“Pamoja na kuvunja rekodi na pia mafanikio ambayo wimbo huu umeleta na unaendelea kuleta, eti kuna watu buku mbili hawakuuelewa,” aliandika Ben Pol Insta kwa ishara ya kushangaa. “Hapo ndiyo utaamini kwamba haiwezekani kuwafurahisha watu wote Duniani, lazima atatokea/watatokea vichwa ngumu kadhaa tu ambao hawatakuelewa unachofanya, FOCUS, Stick to your plans, Move forward, Conquer #HappyNewYear,”
Muimbaji huyo ambaye mwaka 2016 alifanya vizuri na wimbo ‘Moyo Mashine’ ameachia wimbo wake mpya ‘Phone’ akiwa amemshirikisha Mr eazi.


Tag : lainnya
Back To Top