Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli ameviagiza vikosi vya Usalama Barabarani kuwashughulikia wanaoingiza magari kwenye njia za mwendokasi kwani wanavunja sheria za nchi.

Rais huyo ameyasema hayo Jumatano hii jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa magari hayo, eneo la Gerezani, Kariakoo huku akiagiza watakaokiuka wakamatwe na kupelekwa vituo vya polisi ama kung’oa matairi kwenye magari yao ili liwe fundisho kwao na kwa wengine.
“Trafiki mkiona pikipiki, gari linatumia barabara hizi za mwendokasi yashikeni pelekeni kituo cha polisi, yatoeni matairi ili wajifunze. Saa nyingine ukitumia sheria tu watu hawajifunzi lazima mtumie nguvu za ziada ili waziogope hizo barabara za mwendokasi,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amezindua rasmi miundo mbinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (mwendokasi), awamu ya kwanza.

Tag :
lainnya