Na.Vero Ignatus ,Arusha
Tamasha la Arusha tourism marathon limefanyika Leo jijini Arusha ikiwa ni awamu ya pili kufanyika mkoani haha ambapo mashindano hayo yameandaliwa na Arusha Media, Shahanga sport promotion Chini ya udhamini wa Tanapa.
Tamasha hilo limewashirikisha wanariadha kutoka mkoa wa Arusha, Manyara,pamoja na Kilimanjaro ambapo tamasha hilo likiwa limebeba kauli mbiu ya piga vita ujangili, tembelea Hifadhi zetu.
Mgeni rasmi katika tamasha hilo ni Afisa michezo wajiji la Arusha Benson Maneno ambapo amesema kuwa riadha imeutoa mkoa wa Arusha kimasomaso na Tanzania kwa ujumla michezo mingine bado imedorora
Amekipongeza chama cha riadha mkoa wa Arusha na kuwataka kuongeza juhudi zaidi kwani michezo ni ajira,hujenga mwili kiafaya ,pia michezo humtambulisha mtu kitaifa na kimataifa pia, amewataka vijana kuchangamkia fursa hayo.
Katibu wa riadha mkoa wa Arusha kuwa Alfred Shahanga ambapo pia ni muandaaji mwenza wa Arusha Tourism Festival amesema kuwa mashindano hayo yalianza mwaka 2015 walianza na mbio za barabarani huku safari hii wameamua kurudi uwanjani ili kuhamasisha mbio fupifupi ambazo kuwamuda mrefu zimesahaulika.
Tag :
lainnya