Serge Aurier anaendelea kuisumbua klabu kubwa kubwa, baada ya Barcelona ni zamu ya Manchester zote mbili kuweka jitihada kwa ajili ya kumsajili alfubeki ya upande wa kulia wa Paris Saint Germain raia wa Ivory Coast.
Kwa mjibu wa Infosport+, klabu hizo mbili kubwa za Uingereza, zinakuja juu kwa kumuwania mchezaji Aurier. Hakika wajumbe wa Manchester United walikuwepo wakati wa mechi kati ya Ufaransa na Cote d'Ivoire kwajili ya kumchunguza Serge Aurier.
Upande mwingine, Manchester City imeingia kwenye arakati hiyo ya kumtafuta mchezaji Aurier. Pep Guardiola kocha wa Citizens tayari ameanza kuwasiliana na wakilishi wa mchezaji kwa niya ya kumsajili msimu ujao.
Klabu nyingine zinazo muwania Aurier ni pamoja na Naples na Atletico Madrid. Itakuwa vigumu PSG kumziwia mchezaji wake katika majira ya usajili.