Muimbaji huyo amedai hizo asilimia 25 za mapato za wimbo ‘Salome’
ambazo zilielezwa na viongozi wa WCB hazijui kwa kuwa hakuhusishwa
kwenye hilo.
“Tatizo limekuja kwa meneja wangu aliyempatia Diamond kazi, mimi
nimempatia bure Diamond hiyo kazi aitumie,” alisema Saida katika runinga
ya KUTV ya nchini Kenya. “Lakini kwenye kusikia masikioni kwangu na
kwenye vyombo vya habari kwamba Diamond amempatia pesa milioni 25 meneja
wangu wakawa wametengeneza mkataba kwamba huu wimbo utatumika hivi na
hivi ila mimi kama mimi huo mkataba siujui na wala sikuuona na wala
hawakunionyesha. Mimi ninachojua nimempatia kazi Diamond bure ili
aitumie tuinuane wasanii wa Tanzania,”
Pia muimbaji huyo amedai yeye alishiriki kiasi fulani katika kuandaa kiitikio cha wimbo huo kwa kuingiza sauti yake.
Diamond na uongozi wake baada ya kuachia wimbo huo, walionyesha
picha wakati wakifanya makubaliano na meneja wa zamani wa Saida.
“Kitu tulichokifanya kabla ya kurelease wimbo, tulizungumza na
uongozi wake, tukawaambia tunafanya hiki na hiki na kuna kiasi pia
tukakitoa ili kiende kwake halafu tukampa 25% ya publishing. Kila income
ya publishing ikiwa inaingia katika huu wimbo, mama atakuwa anapata
percent,” Diamond alikiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.
Tag :
lainnya