Raisi wa Shirikisho la karate nchini Tanzania na mwenyekiti wa chama cha karate mkoani Kilimanjaro Sensei Kalonga amesema kuwa vijana hao wamepata mafunzo kwa mwaka mmoja na niutaratibu wa chama cha karate.
Kalonga amesema kuwa wameandika historia mpya kwa kuupigania mchezo wa karate mkoa wa kilimanjaro na Tanzania nzima,pia umuhimu wa maendeleo ya vijana kupitia mchezo wa Karate,amesema mchezo huo ni taaluma ndiyo maana wamekaa darasani na kufuzu.
"tumieni mafunzo mliyoyapata vizuri mahali popote mtakapokuwepo zingatieni nidhamu ,upendo pamoja na maadili yote mliyofundishwa huku mkiwa mfano bora wa kuigwa katika jamii,nyie ndio mkataokuwa barua ya kusomeka kwa jamii kuwa karate siyo mchezo wa kihuni
Makamu mwenyekiti wa cha Karate mkoani Kilimanjaro Sensei Hamza Mzonge amesema kuwa karate siyo mchezo wa kihuni kama baadhi ya watu wadhaniavyo,bali msingi mkuu wa Karate ni Nidhamu ,moyo safi,na kuiheshimu jamii kwa ujumla pamoja na familia kwa ujumla.
Sensei Hamza amesema kuwa karate inatengeneza afya ,kudumisha nidhamu,karate haitumiki kuvunja nidhamu ,bali ni mchezo kama michezo mingine na unakanuni zake ,ni tofauti na vile ambavyo watu wandhania lazima uheshimiwe na kila mwanakarate.
"Tunaposema karate haina kufuzu ni kweli ,maana mie mwenyewen ni mkufunzi lakini hadi leo bado naendelea kujifunza siku zote,tudumishe nidhamu,mtu yeyote yule anayevunja nidhamu katika karate siyo katateka alisisitiuza sensei Hamza.
Kwa upande wake sensei Ibrahim Mganga amewataka wahitimu hao kuwa mfano bora haswa katika kuwa na moyo safi huku alisisiktiza kuwa karate ni nidhamu na moyo safi ndiyo sababu huwa wanavaa mavazi meupe kama ishara ya usafi.
"tunavaa mavazi meupe hili vazi linaonyesha usafi na mara zote ukivaa nguo nyeupe utajilinda ili usilitie doa maana litaonekana na kuweka dosari,hivyo basi karate ni zaidi ya vazi jeupe msitumie karate vibaya ikaja ikaonekana ni ya ovyo ndiyo sababu karate siku zote msingi wake ni NIDHAMU"alisisitiza sensei Ibrahim
Tag :
lainnya