Mchezaji wa kimataifa raia wa Republic of Burundi akiichezea A.S.A.S DJIBOUTI TÉLÉCOM ya Djiboutie, Lucho Haruna, amepatwa na jeraha ususoni ni baada ya kuifungia bao moja kati ya mabao matatu dhidi ya AS Port(3-1) kwenye dakika 27 na kupelekwa nje kwa kupata matibabu.
Beki huyo raia wa Burundi, alijiunga na A.S.A.S DJIBOUTI TÉLÉCOM msimu huu, alizidi kuamiwa na kocha wake kwa kuwekwa katika kikosi cha kwanza, inawezekana wakamkosa katika mechi mbili zinazo salia uku wakiwa kwenye arakati ya kutawaziwa wabingwa wa Ligi Kuu nchini hapo.
A.S.A.S DJIBOUTI TÉLÉCOM kwa kuifunga As Port bao tatu kwa moja (3-1), wamechukua nafasi ya kwanza kwa mda wakiongoza Ligi kwa utofauti ya pointi moja tu (1) kati yao na AS Port.
Tuwakumbushe kwamba timu ya A.S.A.S DJIBOUTI TÉLÉCOM inamiliki wachezaji kutoka Republic of Burundi watatu, Nzokira Jeff ambae ni golikipa namba moja wa timu ya taifa kwasasa, Beki mahiri Lucho Haruna na kiungo Moussa Mossi Hadji.