KATIKA kutambua uhusiano mkubwa uliopo baina ya Tanzania na China Kampuni ya Startimes imezindua filamu ya kichina kwa mara ya kwanza na inatarajiwa kuonyeshwa katika Jumba la Sinema la Quality Centre.
Filamu hiyo ijulikanayo kama Goodbye Mr Looser yenye maudhui ya kichina pamoja na tafisri ya maandishi kwa kiswahili inakuwa ni mara ya kwanza kuonyeshwa kwenye jumba la sinema kwa hapa nchini kwani haijawahi kuletwa filamu za aina hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utiaji wa saini wa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Startimes Liao Lanfang amesema kuwa hii ni moja ya hatua kubwa iliyofikiwa hasa baada ya kuona kuwa watanzania wengi wanaangalia tamthilia za Kichina lakini hawajawahi kuona filamu kutoka nchini humo na hii ni fursa kwao kuweza kuiona kwa mara ya kwanza.
Lanfang amesema kuwa jitihada kubwa ziliweza kufanyika kuhakikisha filamu hii inafika nchini Tanzania na imeweza kufanikiwa nakatika filamu hii itakayokuwa na tafsiri ya maandishi ya kiingereza itaonyeshwa kwa mara ya kwanza kwenye Jumba la Sinema la Quality Centre.
Meneja wa Quality Group Utkarsh Garg amesema kuwa katika jumba lao la sinema hakujawahi kuja filamu kutoka nchini China na hii ni mara ya kwanza na itarushwa katika jumba lao na wamefurahi sana kuweza kupata nafasi hiyo.
Mshauri wa masuala ya utamaduni kutoka ubalozi wa China, Gao Wei amesifia kwa hatua hii kubwa kufika hapa nchini kwani anafahamu watanzania wengi wameshazifuatilia tamthilia za kichina kama vile Mau dodo na nyinginezo ambazo zilikuwa zinainyeshwa katika chaneli mbalimbali zinazopatikana katika kisimbuzi cha Startimes.
Tag :
lainnya