Shirika lisilo la kiserikali (SHDEPHA) lililopo wilayani kahama mkoani shinyanga limesema kuwa limeandaa siku maalumu za kutoa elimu ya kijinsia,mimba kwa wanafunzi na ukatili katika jamii ikiwa wilaya ya kahama na mkoa wa shinyanga kwa ujumla unaongoza kwa vitendo hivyo vya ukatili.
Akitoa mpango huo mbele ya wandishi wa habari mkurugenzi wa shirika hilo VENANCE MZUKA amesema wameandaa kwa ajili ya kuielimisha jamii katika masuala ya kijinsia ikiwa vitendo hivyo vimeshamili wilayani humo ambapo watatoa elimu hiyo kwa kushirikiana na ustawi wa jamii ya wilaya ya kahama pamoja na kitengo cha jinsia cha polisi ili kufikisha ujumbe utakaokuwa na mafanikio.
Mzuka amesema katika kampeni hiyo ya utoaji elimu pia wataalam wa shirika hilo watapima watu waliofanyiwa ukatili wa kubakwa,kupigwa,upimwaji wa maambukizi ya virusi vya ukimwi na saikolojia kwa waliofanyiwa vitendo hivyo na kupatiwa ushauri nasaha.
‘’wataalam wetu watapima kwa waathirika wa vitendo hivyo na kuwashauri ili kuwaondolea mawazo waliyonayo ya kujihisi kama wako kitofauti na watu wengine lakini pia tutahitaji watu waafichue wale wote wanaofanya vitendo hivi kwenye jamii maana sisi tunatoa hadi msaada wa sheria mtu kukushika bila ridhaa yako ni kosa’’.amesema mzuka.
Hata hivyo amesema kuwa katika mpango huo pia watahakikisha wanatoa elimu kwa wananchi katika kampeni ya kupinga mimba kwa wanafunzi kwani takwimu za mimba kuanzia mwezi janury hadi mwezi September wanafunzi 21 wa sekondari wameweza kupata ujauzito.
‘katika shule 10 ndani ya mwezi Jan hadi September wanafunzi wameweza kupata ujauzito lakini hiyo sio hali halisi mambo mengi ya hivi yamekuwa yakimalizwa na familia mtu aliempa mimba mwanafunzi anaenda anatoa pesa ya kutosha,pesa za kutosha yanaisha wananchi waseme watu kama hawa na sisi tutasaidia’’.
Na katika hatua nyingine mzuka amesema katika shule hizo za sekondari zenye idadi hiyo ya wanafunzi ni antograhim busoka wanafunzi wawili,seeke sekondari wawili, kishimba sekondari wanafunzi wawili, nyasubi sekondari wanafunzi wawili, nyihogo sekondari mwanafunzi mmoja, mwendakulima sekondari wanafunzi wawili,bukamba sekondari mwanafunzi mmoja na shule inayoongoza kwa idadi kubwa ya wanafunzi wenye ujauzito Jan hadi September ni nyashimbi sekondari yenye wanafunzi saba.
Aidha MZUKA amesema zoezi hilo litakuwa na vituo viwili ndani ya wilaya ya kahama ambapo kituo cha kwanza kitakuwa kakola halmashauri ya msalala na kituo cha pili kitakuwa katika halmashauri ya mji wa kahama ambapo zoezi hilo litaanza Nov 25 na kumalizika Dec 10 mwaka huu.
Tag :
lainnya