Download Mp3 from African

Bwawa la Mindu Morogoro lagundulika kuwa na kipindupindu

Siku moja baada ya mkuu wa wilaya Morogoro Regina Chonjo kuzuia matumizi ya bwawa la mindu  kwa madai kwamba chanzo hicho cha maji kina vimelea vya kipindupindu, diwani wa kata ya Mindu, Hamis Msasa amepingana na maamuzi hayo  na kuruhusu wananchi kutumia maji ya bwawa hilo kwa matumizi yao ya  kawaida  .

Akiongea na channel x  diwan  wa kata ya mindu Hamisi Msasa amesema kuwa  kusimamishwa kwa shughuli za kibinadamu  ikiwemo uvuzi  imekuwa kero kubwa kwa wananchi wake  hasa wakina mama wanaotegemea chanzo hicho  kwa matumizi ya maji huku wananchi hao wakida kuwa  shughuli zote zinazofanyika  katika bwawa hilo zipo kiharali na  wamekuwa wakilinda chanzo hicho  zidi ya waharamia na kumutaka mkuu wa wilaya kufanya  mazungumuzo  na wananchi kabla ya uamuzi  ambao unaweza kuwaasili .

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya morogoro mjini Regina Chonjo amesema kuwa kutokana na hari iliyopo ya dalili za ugonjwa wa kipindu pindu hataweza kuruhusu bwawa hilo litumike mpaka pale watakapo jilizisha kuwa hali imetengamaa kwani katika utafiti uliofanyika asilimia kubwa ya maji ya bwawa la mindu yana chembechembe ya  kuambukiza magonjwa ya tumbo.
Tag : lainnya
Back To Top