Leo nimekusogezea maojiano kati ya Africanmishe na msanii wa Republic of Burundi Flava G Bo, katika arakati ya kujuwa mengi gisi wanavyo endelea kwenye game ya muziki na kipi wanatarajia kufanya hapo baadae pia matatizo na faida gani wanakumbwa nazo kwenye ulimwengu wa muziki.
Msanii G Bo mwenye miaka 25 huku akiwa bado hajajaliwa kuwa na mtoto wala mke alifungukia Africanmishe na kusema kuwa mwaka huu wa 2016 inazidi miaka yote tangu akiwa kwenye game hii ya muziki na kuongeza kuwa mwaka wa 2016 anaweza sema kuwa ameaanza muzki kwasababu kwasasa muziki nikama kazi kwake.
Alipo ulizwa kuhusu kazi zake zote mwaka huu na kipi anatarajia kufanya mwaka ujao, G Bo alifunguka nakusema kuwa
Mwaka wa 2016 nimefanikiwa kurikodi well three na video moja, nimefanikiwa pia kufanya demo nyingi na demo ambayo nilifanya vizuri sana ni demo moja ya kanyosha ilikuwa ni Concour de Dance nilialikwa.
Msanii huyo anayetamba na ngoma yake ‘’Sioni’’ amesema kuwa matatizo ni mengi ila tatizo kubwa ni pindi anapotaka ku shoot video anapata matatizo kwa sababu hajabahatika kupata sponsor ao Manager.
Kinyume na matatizo anayoipata kwenye game ya muziki kuna jambo hapendi huku akiwa wazi nakusema
Kama kuna kitu kinacho nikera zaidi ni promo, promo ipo ila haitoshi, na kitu kingine wasanii wa Republic of Burundi wanazamia ku well kuliko video.
Media zinafanya kazi nzuri ila inabidi wasani tutumike sana, serekali iweke mutisha kwa radio na TV ili ziipe nafasi kubwa Republic of Burundi Flava.
Natarajia kuachia video ya nyimbo yangu ‘’Pam Pam’’ na nina demo mbili ya funga na fungua mwaka. Kuna msanii natarajia kuimba naye ila bado mapema siwezi kumtaja, 2016 sikufanya collabo yeyote ila 2017 nitafanya na wasanii wengi wakubwa. Sijakuwa na mpango wa album labda nikipata manager.
Anaye nisaidia kuniandikia na kukosowa nyimbo zangu ni Djongandio maana mashabiki wanapenda kazi zangu, msanii ninaye kubali Republic of Burundi ni Big Fizzo na nje ya nchi ni Usher.
G Bo alimalizia na kushukuru africanmishe kwa kusapoti muziki wa Republic of Burundi huku akisema kuwa Mishe Mishe itakuwa ya kwanza kupata kazi zake pia akisisitiza kuwa hana bifu na msanii wowote,
Sina bifu na msanii wowote wa hapa ao wa nje ila neno la mwisho naweza sema kwa wale watu wanao nisaidia wasi kate tamaa, wazidi kunisapoti pia nawaambia mashabiki zangu kamwe sitowaangusha mwaka 2017, nawatakia sikukuu njema ya Noeli na mwaka mpya.