Download Mp3 from African

Tambua mengi kuhusu kazi ya muimbaji Papa Fololo mwaka huu na anatarajia nini mwaka ujao

Muimbaji mashuhuri Papa Fololo kutoka Republic of Burundi mwenye makazi yake nchini Canada ambaye azidi kufanya vizuri na kibao chake ''Mapenzi ya Uhakika'' azungumzia kuhusikana na kazi yake ya muziki mwaka huu ilivyokuwa na anatarajia kufanya vizuri zaidi mwaka ujao.

Papa Fololo amefanikisha kurikodi nyimbo xx mwaka 2016 na akadumbuiza demo zaidi ya 33 huku akitamba na nyimbo zake nne (Msaliti, Mama Nihurumiye, Moyo ukipenda na mapenzi ya Uhakika).
Muimbaji huyo alifunguka kuhusu matatizo anazo zipata kwenye muziki akiwa nje ya nchi na kusema

matatizo ni mengi sana hasa mbaya zaidi ni ile ya kunikatisha tamaa na kunivunja moyo kwakile ninachokipenda na kukiweza tokeya ningali mdogo na ikiwa nikipaji niliopewa na Allah. aliongeza pia kinacho nikera mpaka sasa ni wasanii kutosapotiana, bifu za ujinga kati zetu na watangazaji kutokupenda muziki wa nyumbani, kutokuwa na wapromota pia wawekezaji kwenye muziki na kukosa haki ya mauzo kitaifa kwenye kazi zetu za muziki (haki miliki).

Papa Fololo  aligusia pia serekali  huku akisisitiza kuwa serekali inatakiwa ijuwe kuwa wanamuziki nawo nimabalozi wa kuitangaza nchi kwa sura nzuri pia ingesapoti demo na kujipatiya kipato wasanii kupitiya mauzo ya kazi zao na pia kuwachukulia hatuwa wanamuziki wanao kosea mashahiri za mafunzo huku akitowa mfano kwa nchi jirani ya Tanzania inavyo fanya kwa wasanii na akitowa mfano kwa msanii Dully na wimbo wake Nyambizi, Snura (Chura) na wengineo.

Mkali huyo wa ''Mapenzi ya Uhakika'' aliifungukia africanmishe na kusema kuwa anatarajia ku shoot video kali na kuzindua albam ya kwanza ikibeba nyimbo 12.
Aidha, nyimbo yake inayo mtangaza kimataifa kwasasa alisema ni ''Msaliti'' huku akisema kuwa mwaka 2016 alijfunza mengi na kupiga hatua kubwa, msanii huyo yupo kwenye maandalizi ya kufanya collabo na wasanii wawili Chany Queen na Saturday -B na kutowa sababu kuwa ndio wasanii wenye kiwango kizuri chakimataifa.

Msanii huyo kongwe ana wake wawili wa ndoa na watoto wa nne, amesema kuwa kwasasa kuingia studio na mambo mengine anajisaidia pekee yake hana mzamini wowote huku akisema pia amewahi kupata mdhamini aitwaye Pascal Nyabenda kwa bahati mbaya hawakufikia kwenye makubaliano mpaka sasa.

Papa Fololo anawahaidi mashabiki zake kuwapa burudani na kuzidi kuifikisha Republic of Burundi Flava mbali na pia anatarajia kushirikiana na mwanamuziki wa Extra Muzika huku akisema msanii anaye mkubali Republic of Burundi ni sat B nje ya nchi ni Lady Jay D.

Back To Top