Akiongea na Clouds eastward ya Clouds TV, hitmaker huyo wa ‘Mpita Njia’ amedai kuwa Tanzania ni nchi ambayo ina maeneo mazuri yanayofaa kushoot video za uswahilini.
“Nimezaliwa maisha ya uswahilini. Nilipenda kurekodi video yangu Tanzania kwa kuwa hapa kuna mazingira mazuri ya uswahilini. Mwanzo yule manager walivyomleta nikawa simuamini, nilimuona ni mdogo sana kutokana na umri wake,” amesema Alicios.
Muimbaji huyo aliwahi kusema kuwa wimbo wake mpya wa ‘Anita’ ni historia ya kweli ambayo imetokana na wanawake zaidi ya watatu. Alicios kwa sasa ameondoka nchini baada ya kumaliza kushoot video hiyo ya wimbo wake wa ‘Anita’ na manager Joowzey.