Ni muda mrefu msanii huyo amekuwa kimya lakini kwa sasa ameonekana kuanza kuachia kazi zake kwa kasi ikiwa ni siku chache zimepita tangu alipoachia wimbo wake mpya pamoja na video ya ‘Gbagbe Oshi.’
Ijumaa hii Davido anatarajiwa kuachia video ya wimbo wake mpya ‘How Long’ aliomshirikisha msanii kutoka Marekani, Tinashe lakini pia wimbo huo unapatikana kwenye albamu yake mpya, Son of Mercy.
Tag :
lainnya