Msanii chipukizi wa kizazi kipya wa Republic of Burundi Flava, Prince-B Expert ameonesha maskitiko yake kwa niaba ya wasani wote chipukizi kuwa wanazidi kunyanyaswa na kushinda kufikia malengo wakati wanavipaji.
Akiwa studio akirikodi nyimbo yake mpya, ameongea na muandishi wa Mishe Mishe, Prince B amesema "yaani nashindwa kuwaelewa wasani wakubwa ambao ni ma braza wetu kwenye muziki na tayari wamejijengea sifa nyingi nchini wanazidi kutunyima nafasi sisi wasani chipukizi kama present wakati hawana nyimbo mpya pia wanatunyima collabo".
Prince B amefunguka kwanini ma staa ambao ni maarufu wanawanyanyasa na kuwaziwia wasije kuwa juu yawo, upande wake anafikiri kuwa wanaofia wasije kuwazimisha kwenye ulimwengu wa muziki.
"pengine wanaimani mbovu, wanafikiri tutakuja kuwazimisha huku wanasahau kuwa kila kitu na mda wake, bila hivo hata collabo wanatunyima tofauti na nch zingine. Sisi tunahinuliwa na wao kitu moja watambuwe siwezi wataja majina ila wajuwe kama umefanikisha kujenga jina basi nawe pandisha mwingine ili sote tuitangaze nchi yetu", amesisitiza Prince B