Dkt,Egid Mabofu, Kaimu mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya viwango ( TBS) nchini Tanzania. Vero Ignatus Arusha . Wanunuzi wa magari kutoka nchi za nje pasipokupitia kwa mawakala walio na ubia na nchi ya Tanzania kuingia matatani. Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Viwango nchini Tanzania Dkt.Egid Mabofu kwenye mkutano wa wadau uliokutanisha taasisi mbalimbali zinazojihusisha na viwango amesema ikiwa mnunuzi wa gari ataliingiza gari lake nchini bila kupitia kwa wakala watanyang'anywa magari hayo na kuyaharibu au kuyarudisha yalipotoka . Ameainisha nchi za wakala wa uingizaji wa magari nchini alisema ni Uingereza ,Japani ,Dubai ambazo kama magari yatapitia kutoka nchi hizo sheria hazitaweza kuwabana wanunuzi hao Amesema kuwa lengo la kufanya hivyo ,ni kuthibiti uharibifu wa mazingira utokanayo na matumizi ya bidhaa duni zisizokuwa na viwango nchini . Awali amesema, matumizi ya bidhaa duni yamechochea uharibifu wa mazingira na kusababisha kuwepo na madhara makubwa ya uharibifu wa mazingira pamoja na watu Pia amesema ,kama shirika bado linakabiliwa na changamoto ya umuhimu wa matumizi wa bidhaa bora kwa walaji na kusababisha kuwepo kwa kwa ongezeko la uzalishaji wa bidhaa duni nchini "Tunataka walaji au watumiaji wawe wa kwanza kukataa bidha duni ,tunajua wakikataa wao basi mtengenezaji atajirekebisha '"alisema Kaimu mkurugenzi Meneja wa shirika la Mazingira nchini , Clara Makenya ,alisema kama shirika wamejipanga kuhakikisha hadi ifikapo 2030 wameweza kuthibiti mazingira kupitia matumizi endelevu ya bidhaa zenye viwango nchini Dkt.Egid Mabofu amesema ,uharibifu wa mazingira pamoja na kuzagaa kwa takataka kwenye jamii inatokana na utumiaji wa bidhaa duni zinazopelekea kutupwa kiholela mitaani. "Huwezi kununua bidhaa iliyo na kiwango kizuri ukatupa ,kwanza kuisha kazi ,bidha feki ama zisizo na kiwango ni lazima zitupwe kwakua hazikai kwa muda mrefu ,"alisema Clara Pia alisisitiza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya mazingira na viwango vya bidhaa nchini hivyo alisema kama shirika wamejikita katika kuhakikisha kunakuwepo kwa bidhaa zilizo na viwango ili kupunguza uharibifu wa mazingira Meneja wa Viwango nchini ,Mary Meela ambaye pia ni mratibu wa mradi wa utekelezaji wa viwango ,alisema kwasasa kupitia mradi huo wanajianda kutunga sera ambayo itaelekeza udhitibi wa viwango vya bidhaa nchini "Mpaka sasa hatua sera za viwango ama sera za viwango vya chakula ,tunategemea kuwa nazo kutokana na ukutanishaji wa wadau mbalimbali juu ya udhitibi wa viwango nchini,"alisema Mary Meela. |
Tag :
lainnya