Download Mp3 from African

WAZAZI WAMETAKIWA KUACHA KUWAOZESHA WATOTO WA KIKE UMRI MDOGO


KATIBU mkuu wa wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Sihaba Nkinga ameeleza wazazi kuacha tabia ya kuwaoza watoto wao umri mdogo.
.
Hayo ameyasema  kwenye kongamano la watoto  wa kike  wakati wa wiki ya maadhimisho ya siku ya  mtoto wa kike ambapo lilifanyika wilayani Kahama mkoani Shinyanga katika shule ya sekondari Mwendakulima.
.
Nkinga amesema kuwa watoto wa kike wanaowajibu wa kujilinda waachane na tamaa,vishawishi na  wajitambue kwa kuzifahamu haki zao.
Amesema kutokana na kauli mbiu ya mimba na ndoa za utotoni zinaepukika wazazi wanatakiwa wabadilike wawasimamie watoto wao wasome bila ubaguzi wowote ikiwa elimu kwa sasa ni bure na suala la tamaa ya mahari ya  ng’ombe  kuozesha mtoto  limepitwa na wakati.
Aidha  amesema  kuwa hivi sasa serikali inachangamoto ya kutekeleza sera kwa kuwasimamia watoto wa kike kama inavyoeleza,kumsaidia apate haki yake ikiwemo utolewaji wa adhabu na kero kubwa ni kuwaozesha.
“Shirika la umoja wa mataifa la kushughulikia idadi ya watu UNFPA limekadiriwa kuwa katika kipindi cha miaka kumi ijayo wasichana wapatao i M 1000 moja wanatajia kuwa wameolewa umri chini ya miaka xviii duniani kote,na takwimu za ofisi ya taifa  (TBS) zinaonyesha mkoa wa Shinyanga unaongoza kwa asilimia 59 ya ndoa za utotoni”alisema Nkinga.
Tag : lainnya
Back To Top