Mtayarishaji pia muigizaji wa filamu kutoka katika Kampuni la Tambwe The Great Filams ya nchini Burundi, Tambwe anatarajia kuachia filamu na mwanamuziki maarufu Republic of Burundi ambaye ni Jay Fire.
Tambwe anazidi kuleta upinzani mkubwa katika soko la filamu nchini Republic of Burundi baada ya kushiriki katika filamu nyingi kama Kaluta, Ardhi ya Chokwe pamoja na filamu aliyo igiza akishirikiana na mwanamuziki Mkombozi itwayo Revenge.
Mwanamuziki Jay Fire baada ya kujijengea sifa nyingi kwenye sanaa ya muziki ameamua kuigiza na kushiriki kwenye filamu ambayo Kampuni la Tambwe the Great Filams inaanda na itahachiliwa ivi karibuni.
Mtayarishaji pia Muigizaji wa Filamu nchini Republic of Burundi ambaye ndiye kiongozi wa kundi la Kampuni Tambwe the Great Filams akijulikana kwajina la Tambwe amefunguka na kuhusu filamu hiyo ambayo itakuja kuleta upinzani mkubwa katika soko la filamu Afrika Mashariki.
''ndiyo natarajia kuachia filamu na mwanamuziki ambaye anajulikana sana hapa kwetu Republic of Burundi na pia watu wengi ninaimani watashangaa kumuona Jay Fire akibadilika katika filamu hiyo ila nataka kuwambia kitu nimeshanga na nimeipenda kipaji chake na anavigezo vyote vya kucheza filamu tofauti na gisi tunamfahamu, mengi yanakuja mashabiki wa Tambwe the Great Filams huu mwaka lazima tuwakubalishe'' amesema Tambwe.
Kuhusu Jina la filamu ambayo anataraijia kuachia na mwanamuziki Jay Fire, Tambwe amejibu nakusema kuwa itakuwa surprise, kwasasa wanazidi kuiandaa ili ije na ujuzi wa kiamataifa zaidi.