Download Mp3 from African

MCHUMBA WA Baraka da prince ASEMA HAITAJI KIKI YOYOTE... adai sura yake ni kiki tosha

MWIMBAJI wa muziki wa Kizazi Kipya, Najma Dattan amesema hawezi kutumia “kiki” yoyote kwa ajili ya kupata umaarufu, akidai kwamba sura yake ni “kiki” tosha. Najma ambaye ni mchumba wa msanii Barakah Da Prince, alisema ameamua kuweka wazi jambo hilo kufuatia lawama ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake, zikiwemo za kudaiwa kutafuta “kiki” kwa kuwaharibia wenzake. “Mimi huwa sifanyi kazi kwa “kiki” na kwa sasa chochote nitakachokisema naweza nisieleweke hivyo nimeamua bora nikae kimya tu, lakini ukweli ni kwamba mimi mwenyewe ni “kiki” tosha,” alisema kimwana huyo mwenye asili ya mchanganyiko ya Mhindi na Mbongo. Alikuwa akizungumzia tofauti ambazo zilijitokeza hivi karibuni kati yao na fellow wake wa zamani, Mr. Blue aliyekuwa akiwatuhumu Najma na Barakah kwamba walitaka kumharibia ndoa yake kwa kumzushia mambo ya uongo.
Tag : lainnya
Back To Top